Tazama Harambe ya Uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Msamalia ya Kanisa la KKKT Ngara Mjini Jumapili(Julai 14,2013) ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 6 zilichangwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 15, 2013

Tazama Harambe ya Uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Msamalia ya Kanisa la KKKT Ngara Mjini Jumapili(Julai 14,2013) ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 6 zilichangwa.



Kwaya ya Msamalia ya Kanisa la KKKT Ngara Mjini ikitoa Burudani wakati wa   Harambe ya Uzinduzi wa Albamu yao Jumapili(Julai 14,2013) ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 6 zilichangwa ambapo fedha taslimu ni Shilingi Milioni 4 huku Mgeni rasmi ambaye ni Mjumbe wa halmashauri ya Taifa ya CCM-(NEC) Bw.Issa Samma akichangia Shilingi Milioni 3.7 pamoja na kuwa Mlezi wa kwaya hiyo ili kuisimamia iweze kufikia malengo yake katika uimbaji wa injili (Picha na Shabani Nasibu Ndyamukama).


Kwa maringo ni Diwani Viti Maalum CCM tarafa ya Kanazi wilayani Ngara Mkoani Kagera  akitoka kuitunza Kwaya ya Msamalia wakati wa  Harambe ya Uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Msamaria Jumapili(Julai 14,2013).



Toka kushoto ni mchungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Ngara Mjini Eliabo Rwenda akiwana Mgeni Rasmi ambaye ni Mjumbe wa Halmashauri  ya Taifa ya CCM-(NEC) Bw. Issa Samma ,mchungaji Anania Nkwale na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ngara Bw.hadson Bagege wakiwa katika  Harambe ya Uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Msamaria Jumapili(Julai 14,2013).


Mgeni Rasmi katika uzinduzi wa Kwaya hiyo,Mjumbe wa Halmashauri  ya Taifa ya CCM-(NEC) Bw. Issa Samma akiongea na kuchangisha fedha za kwaya hiyo ambapo aliwataka Watanzania  kudumisha Upendo na ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kijamii na Maendeleo  kwa kuacha kuwekeana vikwazo kwa tofauti zao za kiimani na  itikadi za Kisiasa.




Mdau wa Blog ya Mwana wa Makonda na Mfanya biashara maarufu mjini Ngara Fred Gahanga(aliyekaa) akipokea mchango wa fedha kutoka kwa Bi.Niniani bakari ambaye ni Diwani Viti maalum CCM Tarafa ya Kanazi wakati   Harambe ya Uzinduzi wa Albamu ya Kwaya ya Msamaria Jumapili(Julai 14,2013).

Kwaya ya Msamalia ya Kanisa la KKKT Ngara Mjini ikitoa Burudani wakati wa   Harambe ya Uzinduzi wa Albamu yao Jumapili(Julai 14,2013) ambapo Jumla ya Shilingi Milioni 6 zilichangwa ambapo fedha taslimu ni Shilingi Milioni 4 huku Mgeni rasmi ambaye ni Mjumbe wa halmashauri ya Taifa ya CCM-(NEC) Bw.Issa Samma akichangia Shilingi Milioni 3.7 pamoja na kuwa Mlezi wa kwaya hiyo ili kuisimamia iweze kufikia malengo yake katika uimbaji wa injili na Maendeleo kwa ujumla .

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad