Hivi ndivyo Mhashamu Baba Akofu Severin Niwemugizi wa jimbo Katoli la Rulenge Ngara alivyotoa Daraja la Upadre kwa Shemasi Fortunatus Rweikiza katika Kanisa la Mt. Francisco Parokia ya Biharamulo. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, July 15, 2013

Hivi ndivyo Mhashamu Baba Akofu Severin Niwemugizi wa jimbo Katoli la Rulenge Ngara alivyotoa Daraja la Upadre kwa Shemasi Fortunatus Rweikiza katika Kanisa la Mt. Francisco Parokia ya Biharamulo.


Mhashamu Baba Akofu Severin Niwemugizi wa jimbo Katoli la Rulenge Ngara akingia katika Kanisa la Mt. Francisco parokia ya Biharamulo kutoa daraja la Upadre kwa Shemasi Fortunatus Rweikiza.



Mhashamu Baba Akofu Severin Niwemugizi wa jimbo Katoli la Rulenge Ngara akimuombea kabla ya kumpadirisha Shemasi Fortunatus Rweikiza muda mfupi katika Misa takatifu ya Upadirisho katika Kanisa Katoliki la Mt. Francisco Parokia ya Biharamulo.


Shemasi Fortunatus Rweikiza muda mfupi kabla ya kupadirishwa katika Misa takatifu ya Upadirisho katika Kanisa Katoliki la Mt. Francisco Parokia ya Biharamulo mkoani Kagera.


Askofu Niwemugizi akimwekea mikono Padre Fortunatus  kwa ajili ya Baraka.


Mbele ya Shemasi Rweikiza muda mfupi kabla ya Kupadirishwa, Mapadre walimuombea. Anayeonekana hapo ni Padre Damas Missanga(mwenye miwani) ambaye ni Mkurugenzi wa Radio Kwizera ya Wilayani Ngara Mkoami Kagera.




Hapa (Upadre Fortunatus Rweikiza ) ni baada ya kupadirishwa na kuvalishwa rasmi Mavasi ya Upadre  na Askofu Niwemugizi ambaye ni Askofu wa Jimbo la Rulenge –Ngara .


Baada ya Kupewa Daraja la Upadre (Upadre Fortunatus Rweikiza ) akaombewa ili kuitenda kazi ya utume vizuri.


Askofu Niwemugizi akimpaka mafuta ya Krisma aliyekuwa Shemasi Fortunatus Rweikiza.


Askofu wa jimbo la katoliki la Rulenge-Ngara Mkoani Kagera, Mhashamu Severini Niwemugizi,Ijumaa ya ( Julai 12,2013) ametoa Daraja la Upadre kwa aliyekuwa Shemasi Fortunatus Rweikiza.




Misa takatifu ya Upadirisho kwa Padre Fortunatus imefanyika katika Kanisa Katoliki la Mt. Francisco Parokia ya Biharamulo.




Aidha katika hatua nyingine Askofu Niwemugizi ametoa wito kwa waumini wa Kanisa hilo kujenga tabia ya kufunga ndoa na kuachana na dhana visingizio vya gharama kwa  ajili ya harusi, na kuwataka wazazi kuhimiza watoto wao kufunga ndoa na kukemea vikali visingizo vya mahari kwakuwa mambo hayo hayana uhusiano na Kanisa .




Picha Na: .ngarakwetu.blogspot.com.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad