Ndugu yake
Ngeze mwl Damiani Ngeze ambaye ndiye mwanzilishi wa kuishi eneo la Mugunzu
kijijini humo akitoa ushuhuda katika mkutano huo na kukana kuwa ardhi hiyo haikutolewa kwa utaratibu.
|
Mwenye sweta
la njano ni aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Rulenge kati ya mwaka 1977 hadi
1988 Bw Michael Rudigaje akiwa katika mkutano huo na kusema kwamba ardhi hiyo
haikutolewa kwa utaratibu .
|
Wananchi
wa kijiji cha Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera wamemtaka mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoani
Kagera Bw Pius Ngeze kuachia sehemu ya ardhi anayomiliki kijijini humo kwa kuwa
aliipata kinyume na utaratibu.
Wakiongea
(Julai 10,2013 ) katika mkutano wa
hadhara uliohudhuriwa na Wajumbe wa Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya
pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ngara Bw.Deogratias Ntukamazina ,Wananchi hao walisema
wanataka ardhi hiyo kujenga shule ya msingi na kupata sehemu ya makaburi.
Mmoja
wa wananchi hao ambaye ni mjumbe wa serikali ya kijiji Bw Said Biveve alisema wananchi wanahitaji
ardhi kwa ajili miradi ya maendeleo na kwamba ardhi hiyo ilipatikana kwa Ngeze kutumia madaraka kinyume cha sheria
akiwa mwenyekiti wa CCM mkoani Kagera.
Naye
Martin Mwampamba alisema kuwa kinachohitajika ni Maendeleo wala jamii ya Warulenge
haihitaji ruzuku ya serikali katika kujenga shule ya msingi ambapo katika shule mama ya Rulenge
ina msongamano wa wanafunzi wapatao 1437 na kukosa vyumba vya madarasa .
Akijibu
hoja za Wananchi hao Bw Pius Ngeze alisema kuwa alipata ardhi hiyo ikiwa ni
pori lisilokuwa na watu ,yeye na ndugu zake tisa waliokuwa na familia ya watu
30 mwaka 1983 na walianza kuishi katika eneo hilo mwaka 1984 baada ya kupata
barua ya kukubaliwa kupewa ardhi hiyo na katibu wa CCM wa Tawi la Rulenge(Jina la katibu huyo
halikujulikana).
Bw.Ngeze
alidai kuwa tangu aishi pale akitokea kijiji na kata ya Muganza iliyopo mpakani
na nchi Jirani ya Burundi baada ya
majambazi kumuua baba yake na kwamba mgogoro huo wa kudai ardhi umeibuka tangu
mwaka 2010 ambapo alifikisha kesi katika Mahakama ya ardhi ya Chato na kupata
ushindi juu ya ardhi hiyo.
Kwa
mujibu wa barua ya kupewa ardhi kama kielelezo cha hati ya Mahakama inaonesha
kuwa ardhi hiyo ambayo haioneshi ni ekari kiasi gani ni mali yake na ndugu zake
japo baadhi yao katika mkutano huo walimkana kwamba anatumia mabavu katika kuimiliki.
Hata
hivyo aliyekuwa mwenyekiti wa kijiji cha Rulenge kati ya mwaka 1977 hadi 1988
Bw Michael Rudigaje na ndugu yake Ngeze Mwl.
Damiani Ngeze ambaye ndiye mwanzilishi wa kuishi eneo la Mugunzu kijijini humo
wamekana kuwa ardhi hiyo haikutolewa kwa utaratibu.
Kwa
upande wake Mkuu wa wilaya ya Ngara Bw
Costantine Kanyasu ameagiza uongozi wa kijiji hicho kwa kushirikiana na
mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Ngara kuomba ardhi kwa Bw Ngeze kuliko kutumia nguvu kwani ardhi hiyo inamilikiwa kihalali
kwa mujibu wa sheria ya mwaka 1999 iliyoanza kutumika mwaka 2002.
Aidha
Bw kanyasu amesema mlalamikiwa licha ya Mahakama kumpatia uhalali wa kumiliki ardhi hiyo hana budi kutumia busara
kuwakubalia wananchi kujenga shule na kupata sehemu ya makaburi ili wajenge
mahusiano mema na jamii inayomzunguka kuliko kuwa na migogoro.
Habari Na :Shaaban Ndyamukama.
No comments:
Post a Comment