Majambazi yateka Magari na Kupora Abiria na Silaha ya Askari Polisi mpakani mwa wilaya ya Muleba na Biharamulo Mkoani Kagera . - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, July 16, 2013

Majambazi yateka Magari na Kupora Abiria na Silaha ya Askari Polisi mpakani mwa wilaya ya Muleba na Biharamulo Mkoani Kagera .




Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema.
Na Shaaban Ndyamukama BIHARAMULO:



Kundi la watu wapatao 15 wanaosadikiwa kuwa majambazi limeteka mabasi mawili ya abiria yanayosafiri kutoka Bukoba kuelekea Dare es Salaam na kupora mali mbali mbali za abiria katika wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera.




Kamanda wa jeshi la polisi mkoani kagera Bw Philipo Karangi amesema tukio hilo limetokea leo July 15, 2013 saa mbili asubuhi kwenye  eneo la mlima wa  simba ulioko katikati ya  pori la hifadhi ya Biharamulo na kujeruhi abiria baada ya kupiga risasi kadhaa kwenye  magari hayo.




Bw Karangi ametaja magari yaliyotekwa kuwa ni RS lenye namba za usajili T. 495 ATG na NBS lenye namba za usajili T 644 BUR na kwamba abiria 13 wamejeruhiwa lakini  12 wamepata matibabu katika Hospitali teule ya ya Biharamulo kisha kuendelea na safari zao.




Amesema kuwa majambazi hao walikuwa na silaha aina ya SMG sita na LMG mbili na katika kuteka magari hayo waliweza kupora silaha aina ya SMG aliyokuwa nayo  askari polisi aliyekuwa amesindikiza moja ya mabasi hayo na kuondoka nayo porini.




Kwa upande wake Mganga mkuu wa haospitali ya Biharamulo Bw Grasmus Sebuyoya amesema majeruhi  mmoja  Fedrick Rugaihula  mkazi wa Bukoba ndiye hali yake sio nzuri baada ya kupigwa risasi kichwani  jirani na shingo na amelwazwa katika hospitali hiyo kwa matibabu zaidi.




Akiongea na mwanahabari hizi kwa njia ya simu kondakta wa basi la NBS Amiri Omari akiwa amefika eneo la Runzewe akielekea Arusha  amesema kuwa majambazi hao lengo lao ilikuwa ni kupata fedha na simu za mkononi.




“Kusema kweli ndugu yangu hali ilikuwa sio kwani walipiga risasi kioo cha mbele ya dreva na abiria mmoja kupatwa jirani na shingo na kuanza kuvuja huku wengine wakichanwa na vipande vya vioo na hapo kusakwa kutaka kuwasilisha fedha”alisema Omari.




Amesema kuwa katika tukio hilo kulikuwa na maroli mawili yaliyokuwa yamesimamishwa na mabasi hayo katika kusimama kujua nini kinaendelea kulitokea purukushani za risasi na abiria kuanza kuporwa mali zao kwenye pori la barabara itokayo Muleba kuingia mjini Biharamulo .




Hata hivyo  kamanda karangi amesema kuwa jeshi la polisi wilayani Biharamulo linaendelea kusaka majambazi hayo katika pori hilo kwa kushirikiana na askari wa wanyamapori katika hifadhi ya wanyama ya Biharamulo ili kuwatiambaroni ili kufikishwa katika mkondo wa sheria .




Matukio ya ujambazi wilayani Biharamulo yamekuwa yakitokea  mara kwa mara katika hifadhi hiyo ambapo changamoto kubwa ni kwa kamati ya ulinzi na usalama  ya mkoa ambayo kwa sasa majeshi yake yako katika mazoezi ya sherehe za mashujaa zinazotarajia kufanyika Julai 25 mkoani kagera.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad