Kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel kwa kushirikiana na shirika lisilo la kiserikali UNESCO wanatarajia
kuzindua radio jamii katika wilaya ya Karagwe mkoani Bukoba mwishoni mwa wiki
hii.
Uzinduzi huo unafatia ushirikiano
kati ya Airtel na UNESCO katika mradi wa kusadia jamii na kufikisha mawasiliano
ya radio sehemu ambazo zina changamoto za huduma za mawasiliano ya radio.
Akiongea kuhusu uzinduzi huo ya
Airtel Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa Airtel Beatrice Singano alisema
“ Mradi huu wa radio za jamii tunaufanya kwa kushirikiana na UNESCO kwa lengo
la kuendeleza na kuboresha huduma za mawasiliano na kuwafikia wananchi wengi
zaidi hususani wa maeneo ya vijijini.
Tumejipanga kufanya uzinduzi wa
ushirikiano wetu na UNESCO na Radio ya FADECO Karagwe utakaofanyika siku ya
Ijumaa tarehe 19 julai 2013.
Mgeni rasmi atakuwa ni mkuu wa mkoa
wa Kagera Luten Fabian Masawe , pamoja na yeye tutakuwa na viongozi mbalimbali
wa serikali watakaohuduria sherehe za uzinduzi huo.
Tunaamii kwa kupitia radio hizi
jamii itabadilika na kupata elimu zitakazosaidia kuleta maendeleo katika maeneo
mbalimbali ya nchi yetu wananchi wengi wana pata habari mbalimbali zikiwemo za
kibiashara, uchumi, kijamii na kisiasa.
Afisa mradi wa habari na mawasiliano UNESCO
Yusuph Al Amin alisema “tunayo miradi mingi ya kusaidia jamii kujikwamua na
hali ngumu za uchumi, kupata elimu bora, uongozi bora , kuachana na mila potofu
na mengine mengi.
Kwa kupitia mradi huu wa Radio tunaoshirikiana na
wenzetu wa Airtel tumeshaona matunda na mafanikio mengi mpaka sasa, lengo letu
ni kuhakikisha tunatatua changamoto zilizopo za kuwapata wananchi habari za
ndani na nje ya nchi na kuwaunganisha na sehemu nyingine za nchi na Dunia.
Akiongea kuhusu uzinduzi wa Radio
jamii Karagwe Mkurugenzi wa Radio ya FADECO Bw Joseph Sekiku alisema “Mpaka
sasa vifaa na mitambo ya mawasiliano ya kisasa imeshafungwa na tuko katika
hatua ya majaribio ambapo tumeshuhudia ufanisi mkubwa zaidi kulinganisha na
awali kwani tumeweza kutanua wigo na kufikia vijiji vingi zaidi”.
nawashukuru sana Airtel na UNESCO
kwa kutufikia na kuwawezesha kuendesha radio yetu kwa ufanisi zaidi. Radio ya
FADECO ilizinduliwa toka mwaka 2007 na kuanza kurusha matangazo
yetu rasmi kwa vijiji vya karibu, changamoto tuliyokuwa nayo ni pamoja na
kurusha matangazo yetu katika vijiji vilivyo mbali zaidi kutoka hapa radioni.
Kwa kupitia mradi huu tumeweaza kuona mfanikio makubwa tayari.
“Tunagemea kuzindua rasmi
ushirikiano wetu na UNESCO pamoja na Airtel siku Ijumaa hapa Karagwe. Nachukua
fulsa kuwaalika wananchi wadau wa sekta za mawasiliano, viongozi mbalimbali
kuhudhuria halfa hii ya uzinduzi na kusherehekea pamoja nasi mafanikio haya”
aliongeza Sekiku.
Mradi wa radio jamii umeanzishwa
mwaka jana 2012 radio zaidi ya 10 katika maeneo mbalimbali ya nchi zitafaidika
na mradi huu kama ilivyo katika Radio hii ya FADECO iliyopo wilaya ya Karagwe
Bukoba.
No comments:
Post a Comment