CHADEMA yapokea msaada wa fedha shilingi milioni 400 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo vijana pamoja na Wanawake Viongozi wa chama hicho. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Tuesday, March 26, 2013

demo-image

CHADEMA yapokea msaada wa fedha shilingi milioni 400 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo vijana pamoja na Wanawake Viongozi wa chama hicho.

.com/simgad/


chademaChama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimepokea msaada wa fedha shilingi milioni 400 kutoka Chama cha Upinzani nchini Denmark cha Conservative People’s Party (CPP), kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo vijana pamoja na Wanawake Viongozi wa chama hicho.




Akizungumza wakati wa kutiliana saini Mkataba wa utekelezaji wa Mradi huo, Katibu Mkuu wa CHADEMA, DK. WILBROAD SLAA amesema awamu ya kwanza ya utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wanachama wake kupitia Baraza la Vijana la Chama hicho, (BAVICHA), pamoja na lile la Wanawake (BAWACHA), inatarajiwa kuanza Machi, mwaka huu.



slaa
DK.  SLAA
Kwa upande wake Mwakilishi wa Chama cha Conservative People’s Party (CPP), ROLF AAGAARD, anaelezea lengo la chama hicho kutoa msaada huo.




Nae Mwenyekiti wa Baraza la Vijana (CHADEMA), JOHN HECHE amesema msaada huo utawawezesha kutoa mafunzo kwa Viongozi wa Baraza hilo katika mikoa mbalimbali nchini.




Chama cha Conservative People’s Party (CPP), kilianzishwa mwaka 1915 na kimekuwa madarakani kwa kipindi kirefu hadi kiliposhindwa katika Uchaguzi Mkuu uliopita nchini.




Habari Na: cloudsfm.




No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *