Rais wa
Kenya Mwai Kibaki amefanya ziara nchini
Tanzania ambayo ametumia kama njia ya kutoa mkono wa kwaheri wakati huu ambapo
kenya inatarajia kufanya uchaguzi mkuu machi 4 mwaka huu.
Moja ya
kumbukumbu kubwa aliyopata katika ziara yake ya kuwaaga watanzania waliopo
jijini Dar Es Salaam ni kupewa jina lake katika moja ya barabara maarufu
iliyokuwa ikijulikana kama Old Bagamoyo Road
na sasa inaitwa “MWAI KIBAKI ROAD".
Rais Kibaki
akiwa na mwenyeji wake Rais Jakaya Kikwete alizindua barabara hiyo Alhamis
yenye jina la barabara ya Mwai Kibaki.
Barabara hii
kwa mujibu wa meya wa manispaa ya Kinondoni Rajab Mwenda ina historia ya kuwa
imepita katika makazi ya Marais wote wa Tanzania tangu muasisi wa taifa la
Tanzania hayati baba wa taifa Mwalimu
Julius Nyerere hadi Rais wa sasa Jakaya Kikwete.
Shughuli
nyingine iliyofanyika katika ziara ya Rais Kibaki nchini Tanzania ni mazungumzo
aliyoyafanya Rasi huyo wa Kenya na wazee wa mkoa wa Dar Es Salaam ambapo Rais
Kibaki alisisitiza kuimarisha ushirikianao wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili ili kuchochea kasi ya
maendeleo katika ukanda huu wa Afrika
mashariki.
Kenya na
Tanzania zimekuwa katika uhusiano mzuri wa muda mrefu ambao umeimarishwa zaidi
hivi sasa katika mtengamano ndani ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki - EAC.
No comments:
Post a Comment