Askofu
Mkuu wa Kanisa la Anglikana,
Dayosisi
ya Dar es Salaam,
Dk
Valentino Mokiwa
|
Askofu
Chimeledya ambaye anakuwa kiongozi wa sita kushika wadhifa huo nchini, aliibuka
mshindi baada ya jina lake kupenya katika hatua tatu za kura.
Akitangaza
matokeo hayo jana (Feb 21,2013)jioni, Katibu Mkuu wa Anglikana, Dk Dickson Chilongani
alisema kanisa hilo halina utaratibu wa kutangaza kura zilizopigwa lakini
akathibitisha kuwa Askofu Chimeledya ndiye mshindi.
Dk
Chilongani alisema kuchaguliwa kwa Askofu Chimeledya ni utaratibu wa kanisa
hilo ambalo hufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano.
Uchaguzi huo
ulianza kwa ibada iliyoongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Dodoma, Godfrey Mhogolo
na baada ya hapo, Msajili wa kanisa hilo, Profesa Palamagamba Kabudi alitangaza
utaratibu wa uchaguzi.
Chilongani
alisema wajumbe 129 walihudhuria mkutano huo kati ya wajumbe 140 waliotarajiwa.
“Kwa kawaida
katika uchaguzi, askofu yeyote mwenye umri chini ya miaka 60 huwa anaweza kuwa
mgombea na katika uchaguzi huo, maaskofu 21 walikuwa na sifa za kugombea,”
alisema.
Dk
Chilongani alisema Askofu Chimeledya alizaliwa mwaka 1957 na alisoma stashahada
ya theolojia katika Chuo cha St. Philipo kilichopo Kongwa, Dodoma.
“Baadaye
alikwenda Kenya na kuchukua shahada ya masomo ya dini katika Chuo cha St. Paul
kabla ya kwenda kusomea shahada ya uzamili katika theolojia Marekani,” alisema.
Askofu
Chimeledya aliteuliwa kuwa Askofu Mwandamizi wa Jimbo la Mpwapwa chini Askofu
Simon Chiwanga mwaka 2007.
Baada ya
Askofu Chiwanga kustaafu Dk Chimeledya aliteuliwa kuwa askofu wa dayosisi hiyo.
Alisema
askofu huyo mpya atawekwa wakfu mwishoni mwa Mei mwaka huu katika ibada
itakayofanyika katika Kanisa Kuu la mjini Dodoma
No comments:
Post a Comment