Watuhumiwa wanne wakiwemo waliokuwa askari polisi kutoka Biharamulo na Kagera waliokamatwa na vipande 18 vya meno ya tembo wilayani Serengeti wamepandishwa kizimbani kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi. - Mwana Wa Makonda
cV7ufzj

Muhtasari

X-BET

MAIN-

Post Top Ad

cV7ufzj

Tuesday, January 15, 2013

demo-image

Watuhumiwa wanne wakiwemo waliokuwa askari polisi kutoka Biharamulo na Kagera waliokamatwa na vipande 18 vya meno ya tembo wilayani Serengeti wamepandishwa kizimbani kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi.

.com/simgad/
polisi_kituo

IGP .Said  Mwema
Watuhumiwa wanne wakiwemo waliokuwa askari polisi kutoka Biharamulo na  Kagera  waliokamatwa na vipande 18 vya meno ya tembo wilayani Serengeti wamepandishwa kizimbani kwa makosa mawili ya uhujumu uchumi.




Waliofikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya hiyoAmoni Kahimba ni  Boniphace John Kurwa(31),Gerard Tuti (33), David Delina(36) wakulima wakazi wa Biharamulo na Bukoba na Zainabu Hamisi Msabaha(26),fundi cherahani mkazi wa Biharamulo.



Mwendesha mashitaka wa polisi Sajenti wa Polisi Paskael Nkenyenge Mahakama  iliyofurika wasikilizaji kuwa katika muda ,siku wala tarehe isiyojulikana watuhumiwa hao walikamatwa kwa kosa la kula njama za kufanya biashara haramu ya nyara za taifa kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu namba 384(16) iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.



Alisema watuhumiwa hao na wengine ambao hawajakamatwa Tuguro Zakayo,Nyarata Mewama,Emanuel Kananjire(Mnyarwanda)ambao wanatafutwa wanakabiliwa na kosa hilo .



Katika kosa la pili Mwendesha mashitaha huyo aliliambia mahakama kuwa  katika kosa la pili kuwa mnamo januari 4,2013 majira ya saa 5 usiku  katika eneo la Morotonga wilayani Serengeti alikamatwa na vipande 18 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kg 104 vyenye thamani ya  T.Shilingi Milioni 66,760,000= kinyume cha sheria.



Alisema kosa hilo ni kinyume na sheria ya kanuni ya adhabu namba 86 kifungu cha 1,2 cha sheria namba 5 ya mwaka 2009 pia kifungu cha 14(d)cha sheria za uhujumu uchumi namba 60(ii) sura ya 200 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.



Kutokana na kosa hilo la Uhujumu uchumi mshitakiwa hakutakiwa kujibu  lolote kwa kuwa kosa hilo mpaka wapate kibali cha mwendesha mashitaka  wa serikali(DPP).



Katika kosa la kwanza washitakiwa wote walikana,na mwendesha mashitaka  akaomba siku nyingine ya kutajwa kwa shitaka hilo kwa kuwa upelelezi  haujakamilika na kuwa dhamana .



Hata hivyo mwendesha mashitaka wa polisi Inspekta Msaidizi Abdallah Idd aliyekuwa akishirikiana na Nkenyenge aliomba dhamana izingatie sheria namba 148 kifungu cha (5)(e)kuwa wadhamini wawasilishe fedha taslimu zaidi ya Tanzania Shilingi Milioni  10 au hati ya mali isiyohamishika.



Hata hivyo Hakimu Kahimba alitaka kujua sharti hilo ni kwa washitakiwa wote ama mmoja  ambapo mwendesha mashitaka Nkenyenge alidai ni kwa mshitakiwa mmoja Kulwa,madai aliyoyakataa kwa madai kuwa yanawahusu  wote.



Mbali na hilo aliwataka warekebishe mashitaka yao kwa kuwa hayaeleweki kwa kutoweka muda na sehemu walikowakamatia inatia shaka ,na kuhoji wamejuaje wanastahili kushitakiwa Mugumu na si kwingineko.



Akitoa masharti ya dhamana Hakimu Kahimba alisema kila mshitakiwa anatakiwa ajidhamini mwenyewe kwa dhamana ya Shilingi Milioni 2 ya maneno,pia mshitakiwa atadhaminiwa na watu wawili wanaoaminika na kueleweka na wawe wakazi wa Serengeti kwa dhamana ya Shilingi Milioni 10 za maneno.



Sharti la tatu wadhamini ambao ni wakazi wa wilaya hiyo wanatakiwa kuweka fedha taslimu milioni 34 mahakamani ama mali isiyohamishika yenye thamani ya zaidi ya tsh,milioni.35.
 


Na kuwa mali hiyo iwe na hati inayotambuliwa na imefanyiwa uthamini na  mthamini anayetambulika na serikali na wala si barua za watendaji ambazo amesema zimechangia watu wengi kukimbia kesi zao na hawaeleweki.



Washitakiwa ,wadhamini na ndugu waliomba mahakama ilegeze masharti kwa  madai kuwa wao ni wageni na hawawezi kuwapata wadhamini wenye sifa  hizo wilayani hapo.



Kabla ya kutoa masharti ya dhamana alitoa angalizo kwa watu  waliojitokeza kuwadhamini washitakiwa hao wakati hawafahamiani na kuwa  watanunua kesi zisizowahusu.



Kesi hiyo imeahirishwa hadi januari 28 mwaka huu itakapotajwa tena na  watuhumiwa wote wamerudishwa mahabusu baada ya kukosa wadhamini wenye  sifa zilizotajwa na Mahakama  na kibali kimetolewa watuhumiwa wengine  watafutwe ili waunganishwe na wenzao.



Kabla ya kufikishwa Mahakamani hapo Tuti na Derina ambao walikuwa  askari upepelezi Biharamulo na Kagera walifukuzwa kazi januari 10,2013  baada ya kupatikana na kosa kijeshi ili washitakiwe kiraia.



 Washitakiwa hao walikamatwa Januari 6,mwaka huu katika nyumba ya  kulala wageni baada ya Kurwa kuwataja na kubainika kuwa walikuwa askari kanzu  kutoka Biharamulo na Kagera ambao ni D/c Gerard Tuti mwenye namba za F5553  ambaye ni mpelelezi katika ofisi ya kamanda wa  makosa ya jinai wilayani Bukoba .



Askari mwingine ni D/c koplo David Delina mwenye namba E9172 kutoka  ofisi ya upelelezi Biharamulo ambao walikuwa na gari  aina ya Toyota  Ballon lenye namba za usajiri T403 BJK mali ya mtuhumiwa David.



Mtuhumiwa mwingine ni  Boniphace John Kurwa(31) ambaye ni raia mkazi wa Geita ambaye alikuwa na pikipiki  yenye namba za usajili T784 CCC aina ya Sunlog.



Ambaye akiwa na mwenzake aliyetajwa kwa jina moja la Nyarata akiwa na  pikipiki yenye namba za usajili T 834 BPH Toyo ambaye alitelekeza pikipiki na mizigo na kutokomea walikuwa wakitokea kijiji cha  Rwamchanga wakiwa na meno hayo ambayo ni sawa na tembo watatu.



Januari 10 mwaka huu askari hao walifukuzwa kazi rasmi baada ya  mashitaka ya kijeshi kukamilika na kubainika kuwa walitenda kosa la  jinai na hatimaye januari 14 mwaka huu wakapandishwa katika mahakama   ya wilaya kujibu mashitaka yanayowakabili.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad

Contact Form

Name

Email *

Message *