
Mwanaume huyo aliyejulikana kwa jina moja la Mwera (pichani) ambaye
anafanya kazi ya kusukuma toroli stand mpya ya Misuna,inadaiwa usiku wa
kuamukia leo wakati akijaribu kuingia ndani ya nyumba ambayo ipo kwenye hatua
za mwisho mwisho kukamilika kupitia dirishani, miguu yake ilinasa kwenye nondo
za dirisha na kushindwa kuingia ndani.
Baada ya
kushindwa kuingia ndani,wakati akitaka kutoa kwa nguvu miguu yake iliyonasa
kwenye nondo,mikono yake iliteleza na kusababisha aning’ing’e kichwa chini na
miguu ikiwa juu dirishani kuanzia alfajiri hadi aliponasuliwa saa mbili kasoro
robo asubuhi.
![]() |
Picha ya pili,baada ya mpiga picha hii kumvua fulana yake kwa nguvu na sura yake kuonekena.Picha na Nathaniel Limu. |
Baadhi ya
wakazi wa manispaa ya Singida wakimshangaa mwanaume huyo huku akijaribu kuficha
uso wake.
Alinusurika kuuawa baada ya mpiga debe mmoja Sele,kuwasihi watu hao
ambao tayari walikuwa wamebeba silaha za jadi.
No comments:
Post a Comment