Pendelea
kula samaki upate faida zake katika kujenga mwili wako ,kwani
-Huendesha
mfumo wa kinga ya mwili
-Huzuia
saratani
-Hutoa
ahueni kwa wenye pumu
- Hupambana
na dalili za awali za ugonjwa wa figo
-Huyeyusha
damu, huifanya kuwa nyepesi
- Huilinda mishipa ya damu isiharibike
-Huzuia damu
kuganda
-Hushusha
shinikizo la damu
-Hupunguza
hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo na kiharusi
-Hutuoa
ahueni kwa wenye ugonjwa wa kipandauso
-Husaidia
kuzuia uvumbe mwilini.
Karoti |
Karoti
inaweza kuliwa mbichi, kupikwa na kuchanganywa na mbogamboga, kutengenezwa
saladi na juisi. Faida zinazopatikana kutokana na utumiaji wa karoti ni
kuongeza vitamini “A” ambayo inatokana na beta-carotene iliyomo ndani ya karoti
na pia huongeza vitamini B, C, E na madini ya chuma mwilini.
Karoti ina
protini kidogo na haina mafuta ukilinganisha na mazao ya jamii ya kunde na
yenye asili ya uwanga. Vile vile karoti ina nyuzi nyuzi (fiber) ambazo ni
muhimu kwa kukinga kuta za utumbo na kulainisha choo. Karoti inasaidia kuongeza
nuru ya macho, kukinga maradhi ya ngozi, magonjwa yenye asili ya kansa na
kupunguza tindikali inayodhuru tumboni.
Inawezekana ukawa ni mvivu kuandaa juice si vibaya ukatumia matunda kama kifungua kinywa changanya matunda ya aina mbalimbali. |
Juice ya matunda mbalimbali. |
JUICE YA KUTENGENEZA MWENYEWE NI NZURI ZAIDI KWA
KUTUMIA HASA MATUNDA YA AINA MBALIMBALI, Pia kumbuka kwa kuifanya JUICE kama
kifungua kinywa ambapo husaidia kujenga afya
iliyobora pia ni nzuri kwa wale
waliokuwa na nia ya kupunguza uzito na wanashauriwa kupendelea kunywa juice kuliko chai au maziwa.
Kachumbari |
Kachumbari
ni moja kati ya vionjo katika chakula wengi hupenda kutumia kachumbari yenye
mchanganyiko wa matunda ya aina mbalimbali kama nyanya, vitunguu maji, tango,
parachichi, kabichi nk, kwa kuchanganya matunda haya unapata virutubisho vya
asili katika mwili wako.
Vyakula vya aina mbalimbali |
Unaweza kula
kachumbari na vyakula vya aina mbalimbali kama pilau, ugali, ndizi, chipsi nk.
lakini kwa waleambao wanapenda kupunguza uzito unaweza kufanya kachumbari kama
chakula cha mchana kwa kuchanganya matunda ya aina mbalimbali.
Kwa kawaida,
tunatakiwa kula matunda na mboga za majani kila siku, kiasi kisichopungua milo
mitano.
Lakini kwa bahati mbaya sana, siyo watu wote
wenye fursa ya kupata na kula matunda kila siku. Hata wale wenye fursa hiyo,
hawali inavyotakiwa.
Kitendo cha
kutokula matunda hukosesha miili yetu virutubisho muhimu vya kujenga na
kuimarisha kinga ya mwili, matokeo yake miili yetu inakuwa haina kinga ya
kutosha.
Mwili unapokuwa na kinga dhaifu, ni rahisi
kushambuliwa na maradhi hatari, ikiwemo saratani, ambayo kinga yake kubwa iko
kwenye ulaji wa matunda na mboga za majani.
Utashangaa
kuona mtu anamaliza mwezi mzima hajala hata tunda moja. Msimu wa machungwa, kwa
mfano, unaingia mpaka unaisha hajala hata chungwa moja. Ukija msimu wa maembe
nao ni hivyo hivyo.
Kuna mazoea
ya kuona matunda siyo sehemu ya vyakula muhimu. Tabia hii ndiyo chanzo cha
magonjwa mengi yanayotukabili hivi sasa.
Kwa upande
mwingine, kuna makosa hufanyika wakati wa kula matunda. Kitaalamu inashauriwa
kula matunda tumbo likiwa tupu, yaani kabla hujala kitu chochote tanguliza
matunda kwanza na baada ya nusu saa au saa moja, ndiyo unashauriwa ule mlo wako
kamili.
Nimeipenda hii mada ya vyakula huyo samaki wewe!!!
ReplyDelete