LIGI KUU ENGLAND: Msimu 2012/13 kuanza Jumamosi! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 17, 2012

LIGI KUU ENGLAND: Msimu 2012/13 kuanza Jumamosi!

Siku chache tuu baada ya mashetani wekundu Manchester United kumnasa rasmi aliekuwa Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie, Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England kwa Msimu uliopita na Msimu mpya wa Mwaka 2012/13 ukiwa unaanza Jumamosi Agosti 18, Meneja wa Klabu Bingwa England Manchester City, Roberto Mancini, ameonyesha kugwaya na usajili huo na kukiri usajili huo utaiboresha na kuiongezea nguvu Manchester United.


Wiki iliyopita Mancini alikiri Manchester United ina nafasi kubwa ya kuutwa Ubingwa na leo akiongea na Wanahabari kuhusu Mechi yao ya Ufunguzi wa Ligi Kuu England alisistiza msimamo wake huo hasa baada ya Man United kumnunua Nahodha wa Arsenal, Robin van Persie.


Mancini alitamka: “Ni wazi Manchester United wao wana nafasi kubwa ya kuutwaa Ubingwa. Wao wamekuwa wakigombea Ubingwa kila Msimu kwa Miaka 20. Ingawa tumeshinda Msimu uliopita lakini hiyo haibadili wao kuwa ndio Timu inayotegemewa kuwa Bingwa! Na kwa kumchukua Van Persie, Mchezaji wa kiwango cha juu kabisa, Straika Bora Msimu uliopita, na pamoja na Wayne Rooney watakuwa na Mastraika hatari sana!”


Baadhi ya watu wanasema Van Persie ingebidi aonyeshe upendo zaidi kwa Arsenal, baada ya majeruhi yote ambayo aliyapata. Lakini kama nilivyosema mwanzoni, upendo wa dhati siku hizi unatoka kwa mashabiki tu na hili jni jambo ambalo itabidi likubaliwe.


Kwa kuwaondoa wachezaji kama Ryan Giggs, Paul Scholes pale United na John Terry pale Chelsea, hakuna wachezaji wanaoweza kudumu kwenye timu moja milele.


Arsenal sasa tunajikuta kwenye wakati mgumu.


Klabu imesajili washambuliaji kama Lukas Podolski kutoka Cologne, mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud kutoka  Montpellier na kiungo wa Kispain Santi Cazorla kutoka Malaga, ambao wanaweza kufanya vizuri kwenye EPL.
 

Van Persie alijiunga na Gunners mwezi May 2004, muda mchache baada ya klabu yangu ya zamani kumaliza msimu bila kufungwa katika ligi kuu ya England.


Aidha kila  mwaka baada ya mwaka, wachezaji wakubwa waliondoka ambapo Jens Lehman, Ashley Cole, Sol Campbell, Robert Pires, Thierry Henry na Patrick Vieira wote wakaondoka.


Na tangu awasili kutoka Feyenoord, Van Persie aliweza kushinda kombe moja tu - FA Cup, miaka saba iliyopita.


RATIBA MECHI ZA UFUNGUZI:

Jumamosi Agosti 18

[Saa 11 Jioni]

Arsenal v Sunderland

Fulham v Norwich City

Newcastle United v Tottenham Hotspur

Queens Park Rangers v Swansea City

Reading v Stoke City

West Bromwich Albion v Liverpool

West Ham United v Aston Villa


Jumapili Agosti 19

[Saa 9 na Nusu Mchana]

Wigan Athletic v Chelsea


[Saa 12 Jioni]

Manchester City v Southampton


Jumatatu, Agosti 20

[Saa 4 Usiku]

Everton v Manchester United


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad