Rais
Jacob Zuma wa Afrika Kusini ameelezea kusikitishwa na tukio hilo la mauaji ya wachimba madini 36 wa nchi hiyo na kutoa
wito wa kufanyika uchunguzi wa haraka kuhusiana na tukio hilo.
Aidha
Rais Zuma ametoa amri ya kuundwa tume maalumu ya kuchunguza tukio hilo na
waliohusika kuchukuliwa hatu.
Ripoti
zinasema kuwa, kikosi cha kuzuia fujo cha Afrika Kusini kiliwafyatulia risasi
wafanyakazi wa mgodi wa platinum na kuua watu wasiopungua 36.
Mauaji hayo yametokeakwenye eneo ambapo wachimbaji walipigwa hapo juzi kwenye
mgodi wa Lomin karibu na mji wa Rustenburg Afrika kusini.
Vyombo
vya usalama vya Afrika Kusini vinadai kuwa wafanyakazi wa mgodi huo walikuwa
wamejidhaatiti kwa silaha tayari kushambulia jeshi la polisi.
No comments:
Post a Comment