![]() |
Aidha Fainali
ya Wanawake ya Mashindano ya OLIMPIKI LONDON 2012 itakuwa ni kati ya Mabingwa
wa Dunia Japan na Mabingwa watetezi wa
Olimpiki Marekani ama USA baada ya Timu hizo kushinda Mechi zao za Nusu
Fainali hapo jana kwa Japan kuichapa Ufaransa 2-1 Uwanjani Wembley na USA katika Uwanjani Old Trafford, kuendeshwa mchakamchaka
na Canada wa Dakika 120 kufuatia sare ya bao 3-3 katika Dakika 90 na kupata bao
la 4 na la ushindi katika Dakika ya 122 na Sekunde 28.
USA ambao wamecheza Fainali zote za Olimpiki tangu
kwa Soka kwa Wanawake iingie kwenye Michezo ya Olimpiki Mwaka 1996 hivyo
kufanya Fainali ya Japan maarufu kama Nadeshiko maana yake ‘UA ZURI la
PINKI’ na USA kuzikutanisha Timu zilizokutana Fainali ya
Kombe la Dunia Mwaka jana na Japan kuibwaga USA kwa Mikwaju ya Penati.
Fainali hii
ni ya kugombea Medali ya Dhahabu,
itachezwa Alhamisi Agosti 9 Uwanjani Wembley na itatanguliwa na Mechi ya
kuwania Ushindi wa Tatu kati ya France na Canada na Mshindi wake atapata Medali
ya Shaba.
Leo
(Jumanne) Usiku ni Nusu Fainali za Wanaume kati ya Mexico na Japan na itafuatia
ile ya Korea Kusini na Brazil.
Olimpiki 2012: Orodha ya medali. |
---|
Nafasi | Nchi | Medali za dhahabu | Medali za fedha | Medali za shaba | Jumla | |
---|---|---|---|---|---|---|
1 | Uchina | 32 | 19 | 14 | 65 | |
2 | Marekani | 29 | 15 | 19 | 63 | |
3 | Uingereza | 19 | 12 | 12 | 43 | |
4 | Korea Kusini | 11 | 5 | 6 | 22 | |
5 | France | 8 | 9 | 10 | 27 | |
6 | Urusi | 7 | 17 | 18 | 42 | |
7 | Italia | 7 | 6 | 4 | 17 | |
No comments:
Post a Comment