Ajali Mbaya yauwa watu 17 Nkasi wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, August 17, 2012

Ajali Mbaya yauwa watu 17 Nkasi wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.

Baadhi ya wananchi wakiangalia gari aina ya lori lenye namba za usajili T 779 BTV lililotumbukia kwenye mto Lukangao jana baada ya kushindwa kupanda mlima na kusababisha vifo vya watu sita hapo hapo na wengine 20 kujeruhiwa vibaya. Picha na Mussa Mwangoka wa Rukwa yetu Blog.


Na Walter Mguluchuma- Rukwa yetu Blog

Sumbawanga.

 

Watu  17 wamefariki dunia na wengine zaidi ya 38 wamejeruhiwa  vibaya baada ya gari aina ya fuso lenye namba za usajiri T 407 TAGO  kuacha njia  katika eneo la lenye  mlima na kupinduka katika kijiji cha Ntalamilia kilichopo katika wilaya ya NKasi Mkoani Rukwa.

 

Hata hivyo mara baada ya ajali hiyo  kutokea majira ya saa moja asubuhi majeruhi wa ajali hiyo walianza kufikishwa katika hospitali ya mkoa wa Rukwa majira ya saa 5 asubuhi kwa ajili ya matibabu huku wengi wao wakiwa wamepoteza fahamu kutokana  majeraha makumbwa waliyoyapata katika sehemu mbalimbali za miili yao.

 

Akizungumza na Gazeti hili kwa njia ya simu  kamanda wa polisi mkoa wa Rukwa Bw Jacob Mwalaunda amekiri kutokea kwa ajali hiyo ambayo  imetokea leo majira ya saa moja asubuhi katika barabara ya Sumbawanga- Kate  iendayo wilayani Nkasi ,baada ya dereva wa gari hilo ambaye pia  ni mmiliki wa gari hilo aitwae George Kanote (50)mkazi wa kijiji cha kate kumshinda  na kuacha njia na kisha kupunduka na kusababisha vifo  vya watu saba hapo hapo ,huku majeruhi wengine wakiongezeka kupoteza maisha kutoka na ajali hiyo.

 

 Kwa upande wake mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa wa Rukwa Dkt Jasper Nduasinde amekiri  kupokea idadi kubwa ya majeruhi waliojeruhiwa vibaya  ambao bado hajajua idadi yao.

 

Kwa upande wa mmoja wa mashuhuda wa ajali hiyo Leonard Kopa licha ya kutoa ya gari lao  kutumika kutoa msaada kwa majeruhi wa ajali hiyo amevilalamikia vyombo vya ulinzi na usalama kwa kushindwa kufika kwa wakati mara baada ya ajali hiyo huku pia akisema kuwa namba za simu za bure zilizotolewa na vyombo hivyo muda wote hazipatikani jambo linalosababaisha ugumu wa utoaji wa taarifa.

 

Lakini  dunia adaha walimwengu shujaa katika hekaheka za kupokea majeruhi pamoja na miili ya wale waliopoteza maisha  kutokana   na ajali hiyo  mama mmoja ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja ambaye alikuwepo katika eneo hilo la hospitali ya mkoa wa rukwa  alitumia muda huokwakuanzakumuomba mungu ili aweze kuwatia nguvu waliopotezandugu zao kutokana na ajali hiyo huku pia akikemea pepo mbaya anayesababisha ajali.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad