Huu ni Ushamba Au..!!! - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Wednesday, August 08, 2012

Huu ni Ushamba Au..!!!

Mwanaume mmoja wa nchini Uingereza ametoa kali ya mwaka iliyosababisha moto mkubwa pale alipotumia microwave kukaushia viwalo vyake vya ndani na soksi zake. 

Aidha Zimamoto nchini Uingereza walilazimika kufanya kazi ya ziada kuuzima moto uliokuwa ukitishia kuiteketeza nyumba kutokana na moto uliosababishwa na microwave ambayo kawaida hutumika kupasha moto vyakula.


Moto huo ulianza kutokana na kitendo kilichowashangaza watu wengi cha mwanaume mmoja ambaye jina lake limewekwa kapuni mkazi wa mji wa Weymouth uliopo kwenye ufukwe wa kusini magharibi mwa Uingereza.


Mwanaume huyo alitumia microwave kukaushia chupi zake na soksi zake mbichi alizoziweka kwenye sahani ya microwave kwa nia ya kuzikausha kabla ya kuzivaa.


Kikosi cha zimamoto cha Dorset kilichoitwa na majirani walioshtushwa na moshi mkubwa toka kwenye nyumba hiyo usiku wa jumatatu, kililazimika kufanya kazi ya ziada kumuokoa mwanaume huyo toka kwenye nyumba hiyo na pia kuuzima moto mkubwa uliozuka kutokana na microwave.


"Ujumbe unaopatikana hapa ni kamwe usijaribu kuweka nguo za aina yeyote kwenye microwave au oven kwa nia ya kuzikausha", ilisema taarifa ya kikosi cha zimamoto cha Dorset.


Source:nifahamishe.com

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad