Watu kadhaa wamenusurika kifo usiku wa kuamkia leo (Agust 16)katika eneo la Mwangata katika Manispaa ya Iringa baada ya lori walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kupinduka .
Ajali hiyo mbaya imetokea eneo la kona ya Mwangata ambapo inadaiwa kuwa dereva wa lori hilo ambalo lilikuwa limebeba kokoto kuendesha lori hilo bila kuzingatia sheria za usalama barabarani na kutaka kukata kona huku akiwa na spidi zaidi ya 100 hali iliyopelekea lori hilo kuacha njia na kupinduka.
Gari la TANESCO Iringa likitoa msaada wa lori lililopinduka usiku wa leo eneo la Mwangata Iringa |
No comments:
Post a Comment