![]() |
Mto Ruvubu ambao huanzia nchini Burundi na kupita Ngara ,kisha kukutana na mto Kagera na kutengeneza maporomoko ya Rusumo-Tanzania. |
Mratibu wa mradi katika shirika la TCRS wilayani Ngara Bw Eveready Nkya amesema baadhi ya maafisa watendaji wa vijiji ni kikwazo cha maendeleo katika vijiji wanavyoviongoza.
Bw Nkya amesema watendaji hao wanafanya kazi kwa maslahi binafsi badala ya maslahi ya jamii wanayoitumikia na hivyo kushindwa kuwa chachu ya uongozi bora.
![]() |
Hali ya ukungu ambao huja wakati wa masika ukiambatana na Mvua wilayani Ngara mkoani Kagera. |
Amesema baadhi ya watendaji wamekuwa wakijaribu kukwamisha mafunzo ya kuwajengea uwezo wajumbe wa kamati za vijiji kwa kuhofia kuwa endapo kamati husika zitapata uelewa zitawabana na kushindwe kufanya ubadhirifu.
Aidha Bw Nkya amewataka watendaji kutambua kuwa wamepewa nyadhifa hizo ili kuwatumikia wananchi badala ya kuendekeza maslahi yao binafsi.
Katika hatua nyingine,Afisa mtendaji wa kijiji cha Kazingati kata ya Keza wilayani Ngara Bw Philip Kasigwa amekanusha madai ya wananchi wa kijiji hicho kuwa anauza ardhi ya wafugaji wa kijiji hicho na kwamba madai ya wananchi hao ni majungu dhidi yake na kwamba hakuna ardhi iliyouzwa .
Hivi karibuni wakazi wa kijiji cha kazingati walimuomba mwenyekiti wa kijiji hicho kuitisha mkutano ili kupiga kura ya kutokuwa na imani na mtendaji huyo kwa madai kuwa anajihusisha uuzaji wa ardhi ya wafugaji .
![]() |
Makundi ya ng'ombe ambayo huonekana katika ardhi na mapori mbalimbali wilayani Ngara. |
No comments:
Post a Comment