Maadhimisho Mtoto Afrika , Ukatili na Kutumikishwa kwa mtoto bado ni tatizo kubwa Tanzania wataka Vikomeshwe’ - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Saturday, June 16, 2012

Maadhimisho Mtoto Afrika , Ukatili na Kutumikishwa kwa mtoto bado ni tatizo kubwa Tanzania wataka Vikomeshwe’

Siku ya mtoto Africa huadhimishwa tarehe 16 Juni ya kila mwaka kwa azimio la nchi 51 wanachama wa uliokuwa Umoja wa Nchi huru ya Africa (OAU) Kukumbuka mauaji ya kinyama waliofanyiwa watoto wa kitongoji cha Soweto nchini Africa ya Kusini mwaka 1976.


Siku hii huazimishwa kwa lengo la kukumbuka mauaji ya kinyama waliyofanyiwa watoto hao wakati wakidai haki zao za msingi na kuwakumbusha  wazazi na jamii juu ya haki na wajibu wa jamii katika kuwalea watoto.


 Vilevile hutoa nafasi kwa watoto kuwakumbusha haki na wajibu wao  kama watoto wa Taifa ili waweze kujua haki zao za msingi.


Imesemekana bado wapo Watoto wengi ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi wa masomo kufanya kazi za nyumbani badala ya kwenda shule hali inayoongeza idadi ya wasiojua kusoma na kuandika.

 

Aidha Watoto  waishio  mazingira    magumu  katika kijiji cha kabalenzi  wilayani Ngara  wameiomba serikali  kuelimisha jamii  ili kuondokana na vitendo vya ukatili  na unyanyasaji   kwa watoto hali inayopelekea kukosa haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na elimu,afya  na malazi.

 

Akisoma  risala kwa niaba ya watoto  wenzake  katika maadhimisho ya siku ya mtoto  wa afrika  mmoja wa  watoto hao   Devid  Gergory   amesema  unyanyasaji   na ukatili  unaofanywa na  baadhi ya wazazi  na walezi ni  moja  ya sababu inayopelekea  ongezeko  la watoto wa mitaani Na kuitaka    jamii  kubadilika  na  kuondokana na vitendo vya unyanyasaji  na ukatili kwa  watoto  na  kuwapa haki zao za msingi.

 

Kwa mujibu wa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira Dk.Makongoro Mahanga , asilimia 18.7 ya watoto wenye umri kuanzia miaka 5 hadi 17 bado wanatumikishwa katika ajira hatarishi nchini licha ya kuwepo kwa jitihad mbalimbali za kudhibiti vitendo hivyo.

 

Amesema takwimu zinaonyesha kwamba watoto hao wanatumikishwa sana katika sehemu mbalimbali kama migodini, majumbani, mashambani, katika shughuli za uvuvi na katika shughuli za ukahaba.Amesema jumla ya watoto milioni 65 wanatumikishwa katika vitendo hivyo katika nchi za Africa  zilizoko katika jangwa la Sahara, wakati watoto milioni 215 wanatumikishwa katika vitendo hivyo duniani kote.

 

Changamoto kubwa inayochangia vitendo hivyo ni umasikini, pamoja na utelekezaji watoto wengine kufiwa na wazazi wao au baadhi ya wazazi kuwafanya vitega uchumi vyao kwa kuwatumikisha katika shughuli za kuombaomba. 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad