 |
Mkuu wa mkoa wa Kagera Mh. Kanali mstaafu Fabiani Massawe
akikabidhi pikipiki kwa wawakilishi wawakurugenzi wa halmashauri za wilaya na
manispaa.
|
Mkuu wa Mkoa wa Kagera amekabidhi pikipiki nane kwa
wakurugenzi wa halmashauri za wilaya na manispaa ya Bukoba kwa ajili ya
kukusanya taarifa na takwimu mbalimbali za kilimo kutoka vijijini katika mkoa
wa Kagera.
Pikipiki hizo zimetolewa na serikali ya Tanzania kupitia
wizara ya kilimo, chakula na ushirika ikishirikiana na shirika la Kimataifa la
uhusiano la nchini Japan (Japan International Cooperation Agency, (JICA) ambalo
limewakilishwa na Bi. Akasaka Kyoko wakati wa kukabidhi pikipiki hizo nane.
 |
Pikipiki
zilizotolewa na JICA
|
Mhe. Massawe pia amewasistiza sana wakurugenzi wa
halmashauri na manispaa kutunza pikipiki hizo na kuzifanyia kazi iliyokusudiwa
na si vinginevyo. Aidha aliwaomba maafisa kilimo watakaozitumia pikipiki hizo
kukusanya takwimu za kweli ili kuondokana na tatizo la takwimu zisizo sahihi.
Pamoja na pikipiki hizo, JICA pia waliendesha mafunzo ya
ukusanyaji takwimu na kugawa kompyuta moja na “flash” moja kwa kila halmashauri
ya wilaya na manispaa kwa ajili ya kukusanya na kutunza takwimu za kilimo
vijijini.
Mkuu wa Mkoa
aliwashukuru JICA kwa kujitolea kuleta maendeleo Tanzania na hasa katika mkoa
wa Kagera. Ambapo pia amewahakikishia JICA kuwa serikali itaendelea kuhamasisha
wananchi kuondokana na kilimo cha kuchumia tumbo na kujikimu na kuhamia katika
kilimo cha biashara zaidi.
No comments:
Post a Comment