Mratibu wa
mradi katika shirika la TCRS wilayani Ngara mkoani Kagera Bw Eveready Nkya
amesema baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa wamekuwa wakiwaonea wananchi
kwa kuwa hawajui namna ya kuwawajibisha viongozi hao wanaposhindwa kuwajibika
ipasavyo.
Bw Nkya
amesema hayo leo katika kipindi cha mada kilichotamgazwa na radio Kwizera
kuhusu tija ya maadhimisho ya siku ya serikali za mitaa nchini.
Amesema baadhi
ya wenyeviti wa vitongoji, vijji na watendaji wa vijiji na kata wamekuwa
wakitumia udhaifu wa wananchi kutotambua haki zao na kuwaendesha jinsi
wanavyotaka wao jambo ambalo ni kinyume na taratibu.
Bw Nkya
amesema juhudi za ziada zinahitajika kwa mashirika mbalimbali kusaidiana na
serikali katika kutoa elimu kwa viongozi wa serikali za mitaa ili kuboresha
utendaji kazi na kuchochea maendeleo ya jamii kwa ujumla.
Kwa upande
wake Afisa mipango wa halmashauri ya wilaya ya ngara Bw Martin Kanyambo amesema
Elimu duni ya uraia kwa viongozi wa serikali za mitaa imetajwa kuwa miongoni
mwa changamoto zinazokwamisha ufanisi katika uwajibikaji wa viongozi husika kwa
wananchi hali inayokwamisha pia maendeleo katika maeneo wanayoyaongoza.
Aidha Bw
Kanyambo amesema kuwa serikali inajitahidi kutoa elimu ya uraia kwa viongozi wa
serikali za mitaa kuanzia ngazi za vitongoji pamoja na wananchi kwa ujumla ili
kurahisisha maendeleo katika jamii.
No comments:
Post a Comment