Na :Shaaban Ndyamukama - Ngara ,Kagera.
Vijana wawili wakazi wa mji mdogo wa Rulenge wilayani Ngara
mkoani Kagera wanashikiliwa na jeshi la polisi wilayani humo baada ya kudokoa bidhaa mbalimbali katika maduka ya wajasiliamali jumatatu wiki hii
Vijana hao ni Shabani Jacobo ( 37) na Godfrey Turbo (27 )
waliingia katika duka la mfanyabiashara Ismail Mulengera wa mji
wa Rulenge kutafuta bidhaa kuwaletea wateja wake na walipofika ndani ya
stoo walianza kukwepesha baadhi ya mali na katika kuficha ndipo wakabambwa na
mwenye duka
Wananchi waliowakamata waliwakuta na katoni mbili za sabuni na makasha mawili ya amila aina ya pasha na kuanza kupata kipondo wameokolewa na polisi jamii kituo cha rulenge na kufungwa kamba kwa ajili ya kuokoa maisha yao na kufunguliwa mashtaka.
No comments:
Post a Comment