Baadhi ya wachimbaji wadogo zaidi ya 1,000 waliovamia kijiji cha Kinyinya wilayani Kibondo mkoani Kigoma wakiendelea na kazi ya uchimbaji na utafutaji madini. Machimbo hayo mapya yaligunduliwa mwezi uliopita katika eneo ambalo lilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari na soko kijijini hapo.
Kaimu Kamishna wa Madini Ally Samaje akijibu maswali ya waandishi wa habari ikiwa ni pamoja na kutoa ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwa kuwa kupitia maonesho hayo ya kikanda, nchi husika zitaweza kuonesha rasilimali zilizopo na kubadilishana uzoefu wa namna ya kuendeleza shughuli za uongezaji thamani katika madini ili kuleta manufaa zaidi kwa nchi husika kwa namna endelevu zaidi. Katikati ni Waziri wa Nishati na Madini Mh. Willian Ngeleja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mh. Adam Malima.
Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kuanzisha na kuimarisha masoko ya ndani ya madini, kuanzisha vyuo vya Kijemolojia na kuboresha mifumo ya kodi na ushuru kwa ajili ya kuimarisha masoko ya ndani.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam , kuhusu maonesho ya ya kimataifa ya vito yatakayofanyika mjini Arusha, Waziri wa Nishati na Madini Mh. Willian Ngeleja amesema mwaka 2010, Wizara ya Nishati na Madini iliunda kamati ya kuandaa maonyesho ya kimataifa ya vito kwa ushirikiano na Chama cha Wafanyabiashara wa Madini (TAMIDA).
Maonesho hayo yajulikanayo kama Arusha International Gem, Jewelry and Menerals Fair (AIGJMF) sasa yatafanyika katika hoteli ya Mount Meru ya Arusha kuanzia tarehe 26 hadi 29 Aprili 2012.
No comments:
Post a Comment