BAADA YA KUTANGAZWA MATOKEO LEO ASUBUHI KATIKA MBIO ZA UCHAGUZI JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI na Habari kubwa ni anguko la CCM kwenye kinyang’anyiro hicho cha kuwania kiti cha Ubunge.. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, April 02, 2012

BAADA YA KUTANGAZWA MATOKEO LEO ASUBUHI KATIKA MBIO ZA UCHAGUZI JIMBO LA ARUMERU MASHARIKI na Habari kubwa ni anguko la CCM kwenye kinyang’anyiro hicho cha kuwania kiti cha Ubunge..


Add caption
John Mnyika na neno lake baada ya Ushindi "Tunawashukuru sana wana Arumeru Mashariki kwa kutuongezea nguvu ya kijana Joshua Nassari. Shukrani kwa wananchi, wanachadema, serikali nk kusimamia katika ukweli wa ushindi huu wa CHADEMA!Viva CHADEMA. Hakuna kulala mpaka......Peopleeee......s.........!"
CHADEMA leo mchana wamefanya Mkutano kuwashukuru wananchi.
Add caption
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC Chama cha Mapinduzi (CCM) Bw.Nape Nnauye akiongea na waandishi wa habari leo katika ofisi ndogo ya chama hicho zilizopo mtaa wa lumumba jijini Dar es salaam,  juu ya uchaguzi mdogo wa ubunge ulifanyika jana katika jimbo la Arumeru mashariki, ambapo mgombea wa CHADEMA Joshua Nasari ameibuka mshindi kwa kura 32.972, chama cha mapinduzi kimekubali  matokeo hayo yaliotangawa na Tume ya uchaguzi leo asubuhi

Nape kwa niaba ya Chama cha Mapinduzi amempongeza kijana Nasari na kusema "Tunampongeza Joshua Nasari na hakuna hujuma yoyote uchaguzi ulikuwa huru na haki", lakini pia akawapongeza wananchi wa jimbo la Arumeru kwani hiyo ndiyo Demokrasia yao.
Ananilea Nkya''Wana Arumeru Mashariki wametoa sauti zao  kupitia  SANDUKU HURU LA KURA. Kwa tafsiri yangu moja ya jambo ambalo wamelizungumza kupitia  sanduku huru la kura ni kwamba HAIKUBALIKI   madaktari wagome.Kisa? Eti,hospitali  za umma hazina dawa wala vifaa kuwezesha  madaktari  kutumia ujuzi wao  kuwatibu wananchi wakati serikali inakusanya kodi wanazolipa wananchi kwa kununua sukari, mafuta ya taa, petroli, kibiriti, nguo,sabuni, magari  saruji, mabati nk.

 Wana Arumeru Mashariki wamepeleka ujumbe mzito  kwa watawala kwamba HAIKUBALIKI wanawake waendelee kujifungulia sakafuni miaka 50 ya uhuru huku viongozi wao wakiumwa  haraka fedha zinapatikana za kuwapeleka nje ya nchi kutibiwa! Lakini zaidi WanaArumeru Mashariki wamepeleka ujumbe kwamba wao hawakubali kutukanwa katika mikutano ya kampeni.
Ananilea Nkya
Executive Director
Tanzania Media Women's Association (TAMWA)
Chanzo: Mtandao wa Mabadiliko
Kura  halali: 60038

Zilizokataliwa 661

Wagombea:

Mazengo Adam (AFP) 139

Charles Msuya (UDP) 18

TLP 18

Kirita Shauri Moyo 22

Hamisi Kiemi 35

Mohammed DP 77

Sumari Solomon 26757

Nassari Joshua 32,972

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad