Eneo la tukio la moto soko la Kigoma kibanda namba 16A ambapo Kikosi cha zima moto wakiwa wamefaulu kudhibiti moto huo katika ajali ya moto katika Soko hilo.
![]() |
Wananchi wakishanga juhudi za polisi na zimamoto wakikabiliana na moto huo huku Freezer linalodhaniwa ndio chanzo cha moto huo hapa chini. |
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya Kihenya amemtaja mmiliki wa duka hilo kuwa ni Faustine Samweli 39, Mfanyabiashara wa Lumumba Road chumba NO.16 kiliungua moto.
Kaimu Kamanda amesema kuwa Chanzo cha moto huo ni Freezer iliyokuwa imeachwa ikiwaka usiku mzima bila kuzimwa hivyo kusababisha chanzo cha moto huo.
Kamanda huyo amesema kuwa Thamani halisi ya mali iliyoteketea bado haijajulikana na uchunguzi zaidi wa tukio hilo bado unaendelea.
Hata hivyo kamanda kihenya amewataka wafanya biashara wa eneo hilo kuhakikisha usalama wa mali zao kabla na baada ya kufanya shughuli zao kuwa waangalifu wakati wa ufungaji wa maduka yao ili kuzuia tukio la aina hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Issa Machibya akitazama juhudi za askari Polisi na Zima Moto wa kuokoa mali na Kufanikiwa kudhibiti moto huo.
No comments:
Post a Comment