Pia Mkuu wa
Mkoa Gaguti alitoa rai kwa wananchi
kuhakikisha wanausimamia mradi huo pamoja na kuwa na wasimamizi wataalamu
lakini pia wananchi wana wajibu wa kutoa taarifa watakapoona
hawaridhishwi na kazi zinazotekelezwa na Mkandarasi watoe taarifa mara moja
kwani mwisho wa siku mradi huo utabaki kuwa wa kwao na ndio wanufaika.
|
Aidha, Mhe. Gaguti aliwahakikishia wananchi kuwa
atashughulikia kero kwa wajasiliamali mbalimbali hasa Waendesha pikipiki
(Maarufu Bodaboda) ili waweze kufanya kazi zao katika mazingira mazuri na
kulipa kodi za Serikali.
Jambo la
pili alilowaasa wananchi ni kuwa atahakikisha anasimamia kwa karibu sana
ulipwaji wa kodi za Serikali kwa kila anayetakiwa kulipa iwe mwananchi
mmoja mmoja,Taasisi au Kampuni ili Mkoa wa Kagera uweze kuongoza katika ulipaji
wa kodi za Serikali kama unavyoongoza kwa kushika nafasi za juu katika elimu
ili fedha hizo zirejeshwe na kufanya shughuli za maendeleo ya wananchi.
Mradi wa
ujenzi wa barabara katika Manispaa ya Bukoba umegawanyika katika sehemu kuu nne
ili kukamilisha kilometa tano ambapo kilometa 1.7 ni barabara ya Nshambya KCDP
itakayogharimu zaidi ya shilingi bilioni 2.1
Aidha, kuna kipande cha Show
kilometa 1.05, Nyangoye kupita Halmashauri ya Bukoba (Chemba) kilometa 1.3 na
kipande cha kilometa 1.95 cha Bin Said hadi Kilimahewa.
Barabara zote zenye
urefu wa jumla ya kilometa 5 zitagharimu jumla ya shilingi bilioni 7.3.
Fedha za
kutekeleza mradi huo wa kuimarisha miundombinu ya barabara mijini ilitolewa na
Benki ya Dunia kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ambapo muda wa utekelezaji wa mradi ni kuanzia Juni 18, 2018 hadi Aprili 17,
2019 ambapo kazi ziatakazofanyika ni kujenga makaravati 17, mifereji ya maji,
kuweka rami nzito na kujenga daraja moja eneo la barabara ya kuelekea ziwani.
|
Katika hatua
nyingine Mkuu wa Mkao Gaguti
alitembelea kiwanda cha BUKOP cha kukoboa kahawa kujionea ukoboaji wa kahawa
unavyoendelea, Pia litembelea mradi wa BUWASA wa upanuzi wa huduma za maji
Ihungo na kukagua Ujenzi wa madarasa yaliyofadhiliwa na Serikali ya Watu
wa Japani katika Shule za Msingi Kashozi na Nyakato Halmashauri ya Wilaya ya
Bukoba, mwisho aliongea na kujitambulisha kwa watumisha wa Halmashauri ya
Wilaya ya Bukoba na Manispaa ya Bukoba na wadau mbalimbali wa maendeleo katika
ukumbi wa chemba Bukoba Vijijini.
|
No comments:
Post a Comment