Muonekano wa
Vyumba Viwili vipya vya Madarasa vilivyojengwa na Jambo Bukoba katika Shule ya msingi Rulenge
iliyopo Mamlaka ya Mjimdogo wa Rulenge wilayani Ngara mkoni Kagera.
|
Muonekano wa
Ndani wa Vyumba Viwili vipya vya Madarasa vilivyojengwa na Jambo Bukoba katika Shule
ya msingi Rulenge iliyopo Mamlaka ya Mjimdogo wa Rulenge wilayani Ngara mkoni
Kagera.
|
Shule ya
msingi Rulenge iliyopo Mamlaka ya Mjimdogo wa Rulenge wilayani Ngara mkoni
Kagera licha ya kukabidhiwa Vyumba viwili vya Madarasa vilivyojengwa na Shirika
lisilo la Kiserikali la Jambo Bukoba la mkoani Kagera kwa gharama ya
shilingi milioni 22,ikiwemo pamoja na
michango ya Wananchi,Wadau wa Elimu na
Mfuko wa Jimbo, inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa 20
hali inayo walazimu Wanafunzi kukaa kwa msongamano darasani.
Mwalimu Mkuu
wa Shule hiyo Mwl.Vitari Nndayilagije
akisoma risala kwa mgeni rasimi ambaye
alikuwa Afisa Elimu wilaya ya Ngara Bw.Gideoni
Mwesiga wakati wa makabidhiano hayo,amebainisha kuwa Vyumba hivyo vitasaidia
kupunguza msongamano wa wanafunzi darasani na kuboresha kiwango cha taaluma.
|
Afisa Elimu
wa Wilaya Ngazi ya Msingi Bw.Gigdeoni
Mwesiga akimuwakirisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Ngara,Bw.Aidan Bahama ,pamoja na kulipongeza
Shirika la Jambo Bukoba,amewataka Walimu na Wanafunzi kuitunza miundo mbinu
hiyo huku akiyataka Mashirika mengine
kuiga mfano wa Shirika hilo kusaidia kupunguza changamoto ya Vyumba vya
Madarasa kwa Shule za Msingi wilayani Ngara kwani mpaka sasa Halmashauri
inaupungufu wa Vyumba 818 vya Madarasa.
|
Picha ya Pamoja.
Naye Meneja
Miradi wa Shirika la Jambo Bukoba Bw.Gonzaga Steven amesema wataendelea
kuziwezesha Shule za Msingi mbalimbali mkoani Kagera
kupitia mafanikio ya michezo
mbalimbali ya Jambo Bukoba ili Wanafunzi wapate kusoma katika Mazingira rafiki.
|
No comments:
Post a Comment