![]() |
Baadhi ya
Miili ya maiti iliyookolewa baada ya ajali kutokea Nanenane Darajani eneo la
Uyole Mkoani Mbeya Jana (Juni 03,2013) .
|
Watu 6
wamefariki Dunia na wengine 6 kujeruhiwa katika ajali ya Barabarani iliyotokea
Nanenane Darajani eneo la Uyole mkoani Mbeya.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mbeya Barakael Masaki amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na
kuwataja marehemu hao kuwa ni pamoja na Dereva mmoja wa Hiace.
Kamanda Barakael Masaki. |
Masaki
amesema dereva wa Hiace amefahamika kwa jina la Meshack Hosea aliye kuwa
anaendesha Gari nambali T 178 AAV aina ya Toyota Hiace iliyokuwa ikifanya
safari zake kati ya Sokomatola na Uyole
ambapo muda huo ilikuwa ikitokea Sokomatola kuelekea Uyole.
Dereva wa
Toyota Land Cruiser Abdalah Ndabagi anashikiliwa na Polisi kwa Mahojiano zaidi.
Maiti nne
hazijatambuliwa hadi sasa wakiwemo wanawake wanne waliokuwa abiria katika
Daladala hiyo na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa jijini Mbeya.
Aidha
amesema majeruhi sita wamelazwa katika hospitali ya Rufaa wakiwemo wanawake
watano na Mwanamke mmoja ,ambao mpaka sasa majina yao hayatambuliwa kutokana na
kujeruhiwaa vibaya.
Chanzo cha
ajali hiyo kimetajwa kuwa ni mwendo kasi
wa Magari hayo na wito ameutoa kwa Madereva kuwa makini na kufuata sheria za
Barabarani ili kuepusha ajali ambazo zingeweza kutokea.
Picha na
Mbeya yetu Blog.
No comments:
Post a Comment