Mara baada
ya Shule ya Sekondari Ihungo kukamilika ujenzi wake kwa asilimia zaidi ya 90% Serikali
tayari imewarudisha Wanafunzi walikokuwa wamehamishiwa katika Shule ya
Sekondari Omumwani katika Manispaa ya
Bukoba na Chuo cha Ruhija Halmashauri ya Wilaya Bukoba ili wakaendelee na
masomo yao katika shule yao ya Ihungo Sekondari.
Katika
kukamilisha ujenzi wa miundombinu midogo midogo iliyobakia katika katika shule
hiyo Mkuu wa Mkoa wa Kagera , Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti alipotembelea Shule hiyo August 25,
2018 , alisema kuwa yeye jukumu lake ni kufuatilia na kuhakikisha kila
kilichopangwa kujengwa katika shule hiyo lazima kijengwe na kukamilshwa na
Kampuni ya Tanzania Building Agency (TBA).
Tetemeko la
Ardhi Mkoani Kagera lilisababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu yote ya Shule
ya Sekondari Ihungo ikiwemo Madarasa, Mabweni, Maabara, Bwalo, Jiko, Vyoo
na Mabafu, Nyumba za Walimu, Jengo la Utawala, Kanisa, Msikiti, Maktaba na
Mifumo ya maji na umeme.
|
Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejenga majengo matatu ya madarasa yenye
ghorofa moja kila moja, kila jengo lina vyumba 8 vya madarasa na ofisi 4 na
kufanya jumla ya vyumba vya madarasa 24 yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 960
na jumla ya ofisi 12.
Serikali pia
imejenga majengo 3 ya mabweni yenye ghorofa 2 kila moja, kila jengo lina uwezo
wa kuchukua wanafunzi 384; hivyo majengo yote 3 ya mabweni yatachukua wanafunzi
1,152, vikiwemo vyoo na mabafu. Serikali pia inajenga nyumba mpya za
wafanyakazi kwa matumizi ya familia 30.
Aidha,
Serikali imefanya ukarabati wa Maktaba ya Shule, Jengo la Utawala, Maabara ya
Kompyuta, Jengo la Kilimo, Bwalo, Jiko na Maabara za Fizikia, Kemia na
Baologia.
|
Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti atembelea Shule ya Sekondari Ihungo
na kuona maendeleo ya ukamilishwa wa baadhi ya miundombinu midogomidogo katika
majengo baada ya Serikali kuamua na kuijenga upya shule hiyo iliyoharibiwa
vibaya na Tetemeko la Ardhi lililotokea Mkoani Kagera Septemba 10, 2016.
|
Tayari Shule
ya Sekondari Ihungo imepangiwa wanafunzi 679 wa Kidato cha Tano na tayari
wanafunzi 556 wameripoti shuleni hapo tangu tarehe 16/7/2018 na wanafunzi
hao ni wa michepuo ya PCB, PCM, CBG, EGM na HGE na wanaendelea na masomo
kadri ratiba ya shule ilivyopangwa.
Ikumbukwe
kuwa Shule Sekondari Ihungo awali kabla ya Tetemeko kutokea ilikuwa ina uwezo
wa kubeba wanafunzi 801 na kwasasa baada ya kujengwa upya inao uwezo wa kubeba
wanafunzi 1,152.
|
No comments:
Post a Comment