Mkuu wa Mkoa
Gaguti alitoa rai hiyo Augusti 24, 2018 katika Kituo cha Afya Kimeya Wilayani
Muleba alipofanya ziara ya kujitambulisha katika Wilaya hiyo na kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo ambapo alitembelea na kukagua ujenzi wa majengo matano
yaliyogharimu kiasi cha shilingi milioni 456 zilizotolewa na Serikali pamoja na
wananchi kuchangia kiasi cha shilingi milioni 11.7.
Mhe. Gaguti aliwashukuru wananchi kuchangia miradi ya maendeleo na kuwataka kuendelea kuchangia miradi mbalimbali ili kujiletea maendeleo na kuitunza pia miradi hiyo. |
Katika hatua
nyingine Mkuu wa Mkoa Gaguti alitembelea shamba la kahawa lenye ekari 45 la
Mkulima Bw. Shakiru Yahya lililoko Kijijini Karutanga kata ya Magata Karutanga
na kujionea kilimo cha Kahawa cha kisasa na chenye tija ambapo shamba hilo ni
la mfano kwa wakulima wengine ambao wanajishughulisha na kilimo hasa zao la
Kahawa.
Akitoa
taarifa kwa Mkuu wa Mkoa Mkulima wa shamba hilo Bw. Shakiru Yahya alisema kuwa
alihamasishwa kulima kahawa na baba yake mzazi wakati akiwa mdogo baada ya baba
yake kuwa analima Kahawa na kuuza na kupata fedha za kuendesha familia ikiwa ni
pamoja na kuwapatia matumizi mbalimbali ya kifamilia na karo za shule.
Baada ya
kujitegemea Bw. Shakiru mwaka 2000 alianza kulima kidogo kidogo na mpaka sasa
amefikisha ekari 45 za shamba la mibuni aina ya Arabika na Robusta na amepata
mafanikio makubwa kwani kwa msimu uliopita aliweza kuvuna tani 40 za kahawa
na kupata fedha za kitanzania shilingi milioni 60, anasomesha watoto
wake, ameajili zaidi wafanyakazi 50, amenunua magari ya kusafirisha mizigo,
amenazisha kiwanda cha kusindika kahawa chenye gaharama ya milioni 650.
Mara baada
ya kutembelea na kukagua shamba hilo , Gaguti aliwataka wananchi wa Wilaya ya
Muleba hasa wanaozunguka shamba hilo kwenda kwa Bw. Shakiru kujifunza kilimo
cha Kahawa badala ya kuendelea kumtazama tu.
|
Katika Ziara
hiyo pia Mkuu wa Mkoa aliweza kuongea na Watumishi wa Serikali, Wazee na Wadau
mbalimbali wa Maendeleo ya Wilaya ya Muleba ambapo aliwakumbusha watumishi wa
umma kuhakikisha wanatatua kero za wananchi kila Mtumishi katika nafasi
yake ili kupunguza migogoro mbalimbali katika jamii na kuwafanya wananchi
waiamini Serikali yao.
Mwisho Mhe.
Gaguti alitoa msisitizo wa kulipa kodi ya Serikali kwa wadau mbalimbali na
wafanyabiasha ambapo alisema kuwa bado hajaridhishwa na kiwango cha ulipaji
kodi katika Mkoa wa Kagera.
Mhe. Gaguti alisema suala hilo ni kipaumbele chake
katika Mkoa na anataka kuona Kagera inaongoza katikaulipaji wa kodi bila
shuruti.
Mkuu wa Mkoa
Gaguti anaendelea na ziara ya kujitambulisha katika Wilaya za Mkoa wa Kagera
ili kuufahamu vizuri mkoa wake na maeneo yake ya utawala lakini paia
anaendelea na ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri za
Wilaya.
|
No comments:
Post a Comment