Serikali
imewaagiza wakuu wa wilaya za mkoa wa Kagera kutenga Zahanati zitakazopokea na
kuwahudumia Wagonjwa wa Homa ya Ebola endapo
watabainika.
Waziri wa Afya,
Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Bi. Ummy Mwalimu akiwa ziarani Jana
August 27, 2018 katika mpaka wa Tanzania na Rwanda eneo la Rusumo wilayani Ngara ili kuangalia ni
kwa jinsi gani mkoa wa Kagera umejipanga kudhibiti ugonjwa huo.
Waziri Ummy
amesema Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa taarifa mpya ya kwamba Tanzania ipo
katika hatari kubwa ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo kutokana na mwingiliano
wa wasafiri kati ya Tanzania na nchi jirani za Rwanda, Burundi, DRC na Uganda.
|
Waziri Ummy Mwalimu akikagua banda maalum kwa ajili ya shughuli zakuwapumzisha raia wa kigeni wanaobainika au kuhisiwa kuwa na dalili za ugonjwa Ebola. |
Hata hivyo
Waziri Amesema Serikali kupitia Wizara ya Afya wameshatoa mafunzo kwa watoa Huduma za
Afya jinsi gani ya kuwahudumia watu wanaohisiwa au wenye ugonjwa wa ebola sambamba
na utoaji wa vifaa kwa ajili ya kinga na kwamba hadi sasa hakuna mtu ambaye
amebainika kuwa na ugonjwa wa ebola hapa nchini Tanzania.
|
No comments:
Post a Comment