Sajida Said
(36), akiwa na mapacha wake hao.
Mkazi wa
Kijiji Lubao kilichopo Kata ya Ijumbi Wilayani Muleba mkoani Kagera, Sajida
Saidi, amejifungua watoto mapacha wenye afya njema katika Hospitali Teule ya
Rubya iliyopo Muleba mkoani Kagera.
Akizungumza
na waandishi wa habari wilayani humo August 27/2018 hii, Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo
Dkt.George Kasibante alisema hali ya mama huyo na watoto wake aliojifungua juzi
ni nzuri.
Watoto hawa
waliozaliwa kabla ya muda wao wanaendelea vizuri na sasa wapo kwenye wodi
maalumu ya joto" alisema Kasibante.
Alisema katika
Hospitali hiyi ili ni tukio la pili kwa mama kujifungua watoto mapacha zaidi ya
wawili kwani mwaka jana kuna mama mwingine alijifungua watoto watatu.
Alisema
uzito wa watoto hao umetofautiana kwani yupo mtoto wa kilogramu 2.1, 2.1 na
2.6.
Mama wa
watoto hao Sajida mwenye wa watoto watano ambapo sasa atakuwa nao nane amesema
anajisikia vizuri kupata watoto hao ukizingatia naye kuwa alizaliwa pacha na
mwenzake aitwaye Shakira Saidi.
|
Tuesday, August 28, 2018
Mama Ajifungua Watoto Watatu Hospitali ya Rubya Muleba, Kagera.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment