Mkuu wa
Wilaya Kinawiro alitoa rai kwa wananchi hasa wazazi wa watoto wanaosoma katika
shule hiyo ya Msingi Kibeta kuacha kuwazuia wanafunzi kwenda shuleni hapo
kuendelea na masomo yao kwani hali tayari imetulia na Jeshi la Polisi
linaendelea na uchunguzi lakini pia Serikali inaendelea kuifanyia kazi taarifa
ya uchunguzi ya Kidaktari iliyotolewa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa
ya Mkoa juu ya sababu zilizosababisha kifo cha Mwanafunzi Spelius Eladius.
“Jana
asubuhi siku ya Jumanne tarehe 28 Agosti, 2018 nilifika Shule ya Msingi Kibeta
na kukutana na Walimu na Wanafunzi niliongea nao na kuwahakikishia kuwa Serikali
inaendlea kufanya kazi kuna kuwataka walimu kuendelea kufundisha na watoto
waendelee kuingia madarasani. Lakini pia leo tarehe 29 Agosti, 2019 nimeenda
shuleni hapo kuangalia hali lakini nimekuta kuna baadhi ya wazazi wamewazuia
watoto wao kwenda shuleni, natoa wito kwa wazazi wawache watoto waende shule
kwani hakuna tishio lolote shuleni hapo.” Alitoa wito Mkuu wa Wilaya Kinawiro.
Aidha, Mhe.
Kinawiro alitoa wito kwa wananchi wa Bukoba kutulia na kuiamini Serikali yao
kwani tukio hilo linaendelea kufanyiwa kazi na taarifa zitakuwa zinatolewa mara
kwa mara na Serikali hasa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa na Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa ili wananchi wajue kila kinachoendelea katika kuhakikisha haki inatendeka
na wananchi wanapata taarifa sahihi jinsi kifo cha mwanafunzi huyo kilivyotokea
na ni nini kilisababisha kifo hicho.
Pia Mhe.
Kinawiro alito wito kwa Walimu katika shule Mkaoni Kagera kuhakikisha
wanatekeleza majukumu yao kulingana na kanuni, taratibu na sheria na kuzingatia
kanuni na miongozo ya utoaji wa adhabu kwa wanafunzi watakaobainika kuwa na
makosa lakini wasichukue hatua za kutoa adhabu holela bila kufauta kanuni za
utoaji wa adhabu hizo na kusababisha madhara kwa wanafunzi.
Mwanafunzi
Spelius Eladius (13) wa Shule ya Msingi Kibeta Manispaa ya Bukoba anasadikiwa
kufariki dunia Agosti 27, 2018 muda mfupi baada ya kupigwa viboko na Mwalimu
Respecius Mutazangira Mwalimu wa shue ya Msingi Kibeta na kusabisha kifo chake
baada ya mwanafunzi huyo kusadikiwa kuwa ameiba pochi ya Mwalimu Elieth Gerald
asubuhi alipompokea Mwalimu huyo mizigo yake lakini baadae ilikuja kugundulika
kuwa hakuwa ameiba pochi hiyo.
Uchunguzi wa
suala hili unaendelea na taarifa zitatolewa na Serikali kadri suala hili
linavyofanyiwa kazi.
|
Wednesday, August 29, 2018
DC Bukoba na Taarifa kuhusu Kifo cha Mwanafunzi aliyefariki kwa kipigo cha Mwalimu.
Tags
# HABARI
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
HABARI
Labels:
HABARI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment