Gari (la
kwanza pichani kushoto ) lililombeba Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.Ummy Mwalimu limepata ajali na kumgonga mwendesha
Baiskeli na kumsababishia majeraha mwilini mwake.
Kamanda wa Polisi
Mkoani Shinyanga Simon Haule amesema
gari hilo lenye namba za usajili STL
2777 Mali ya Wizara ya Afya likiendeshwa na Dereva Bw. Jumanne Ally amemgonga Marko
Charles mkazi wa kata ya Busoka katika Halmashauri ya mji wa Kahama.
Amesema Waziri
Ummy alikuwa akitokea wilayani Ngara
kwenye ziara ya kikazi ya siku moja na kwamba Bw. Marco aliegongwa amepata majeraha kwenge bega na mkono wa
kushoto na amelazwa hospitali ya mji wa Kahama.
Hata hivyo Kamanda
Haule amsema baada ya ajali hiyo dereva ameruhusiwa kuendelea na safari kwani Waziri
anaelekea Dodoma kikazi na uchunguzi bado unaendelea kwani ikithibitika dereva
alifanya uzembe atafikishwa Mahakamani.
|
Thursday, August 30, 2018
Gari la Waziri wa Afya lasababisha Ajali –Kahama.
Tags
# MATUKIO
Sambaza Hii
Chief Editor | Mhariri
MATUKIO
Labels:
MATUKIO
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuhusu Mwandishi
Journalist / Chief Editor / Tanzanian Blogger
Simu: 0756830214 / 0620197747 / 0789925630.
No comments:
Post a Comment