

![]() |
Waziri wa
Nishati, Dkt.Medard Kalemani
akibonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya kuanza kupatikana kwa huduma ya umeme
katika Kitongoji cha Gwingwe ,Kijiji cha Kasharazi wilayani Ngara mkoani
Kagera. Na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Ngara, Michael Mtenjele.
Wakati wa uzinduzi huo Kijijini hapo, Waziri Kalemani amesema ili Tanzania ipate maendeleo ni muhimu vijiji
vyote vikapata umeme wa uhakika.
Amesema ni
vyema sasa wakandarasi waliokabidhiwa jukumu la kusambaza umeme vijijini
wafanye jitihada hizo haraka ili vijiji vyote vipate umeme kwa wakati.
Hata hivyo Waziri Kalemani amewataka wananchi kuitunza vyema
miundo mbinu hiyo kwakua ina manufaa kwao na kizazi kijacho.
Waziri wa
Nishati ilifungua matumizi ya umeme wa Gridi ya Taifa wilayani Ngara,mkoani
Kagera Aprili 8 ,2018 huu hivyo kuwezesha Wilaya hiyo kuachana na matumizi ya
umeme wa mafuta.
![]() |
Pia Waziri kalemani alitembelea na Kukagua Maendeleo ya Mradi wa Umeme Rusumo. |


No comments:
Post a Comment