Waziri Mkuu- ‘’Washiriki UMISSETA na UMITASHUMTA Onesheni Vipaji Viwape Manufaa Kiafya, Kitaaluma na Ajira. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Sunday, June 10, 2018

Waziri Mkuu- ‘’Washiriki UMISSETA na UMITASHUMTA Onesheni Vipaji Viwape Manufaa Kiafya, Kitaaluma na Ajira.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa Jana (Jumamosi, Juni 9, 2018)  amefungua rasmi Mashindano ya Umoja wa Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi na Sekondari Tanzania  (UMISETA) yanayofanyika kwenye  Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Waziri Mkuu amewataka Viongozi wa Mikoa na Wilaya zote nchini wahakikishe kuwa masomo ya haiba, michezo na stadi za kazi yanafundishwa kikamilifu kwenye shule zote za msingi.

 Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema somo la elimu ya michezo kwa Shule za Sekondari nalo lifundishwe kikamilifu na vyuo vya michezo kama Malya viendelee kuwaendeleza walimu wa michezo.
Mashindano hayo yamehudhuriwa na Naibu Waziri waNchi, OR – TAMISEMI, Joseph Kakunda, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wadhamini wa Mashindano hayo, Wadau wa michezo na baadhi ya wananchi wa mkoa wa Mwanza.
Mkurugenzi Nyanza Bottling Company Ltd  Christopher Gachuma akisalimaina na Mh. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Aidha, amewataka wanafunzi wanaoshiriki mashindano hayo watumie ushiriki wao kwa kuuthibitishia umma dhamira waliyonayo ya kuonesha kuwa, zipo fursa nyingi za ajira endapo vipaji vya michezo na sanaa vitatumika kikamilifu. 

Amesema uhalali wa michezo na mashindano shuleni unatajwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015-2020, Sera ya Maendeleo ya Michezo ya mwaka 1995,  Sera ya Elimu ya mwaka 2014 ambazo kwa pamoja zinaelekeza kutambua na kuendeleza vipaji vya wanafunzi shuleni kufikia malengo ya maendeleo endelevu.
 
Kaulimbiu ya Mwaka huu 2018 inasema MICHEZO ,SANAA NA TAALUMA NI MSINGI WA MAENDELEO YA TAIFA .

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Majaliwa amewaagiza Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya wahakikishe maeneo ya michezo na burudani yanapimwa na yasiingiliwe, pia vitengo vya michezo kwenye ofisi za Halmashauri na Mikoa vitengewe fedha za kuendeshea michezo. 
 
Wanafunzi wa UMISETA  wakiimba wimbo wa alaiki uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema Vipaji vya Michezo na Sanaa vitaitangaza nchi kimataifa na kuongeza fursa ya ajira kwa Watanzania.

 Amesema kauli mbiu ya michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA ya mwaka  huu ni “michezo, sanaa na taaluma ni msingi wa maendeleo ya mwanafunzi  katika Taifa letu”. 
Mashindano hayo  yanafanyika kwa mara ya 3 mfululizo katika Jijini Mwanza pamoja na  kampuni ya COCA COLA kwa kudhamini michezo ya mpira wa miguu na kikapu kwa Shule za Sekondari na kampuni ya AZAM kwa kujitolea kuonesha michezo hiyo kwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad