|
Halmashauri
ya Wilaya ya Ngara mkoani Kagera kupitia Idara ya Elimu Msingi, imetumia Maadhimisho ya Wiki ya Elimu
kuhamasisha Jamii kutambua umuhimu na kuongeza ari ya utendaji kazi kwa Walimu
na Wanafunzi wilayani humo.
Akisoma
risala wakati wa maadhimisho hayo,kwa niaba ya Afisa Elimu Wilaya ya Ngara May 30,2018, Afisa Taaluma (W) Bw. Oswald
Rujuba, amesema wameaitumia siku hiyo ili kuihamasisha Jamii kuinua taaluma ya Wanafunzi
wilayani Ngara.
Amesema
maadhimisho ya siku ya kilele cha Wiki ya Elimu yamesimamiwa na idara ya Elimu
Msingi na Elimu Sekondari na kwamba idara ya Elimu Msingi katika wiki hiyo
imefuatilia Maendeleo ya taaluma katika Sule ya za Msingi zipatazo 74.
“Kutokana na
hali ya taaluma wilayani kwetu kushuka; tumetoka nafasi ya Kwanza hadi ya Nane
kimkoa, tuliamua kufanya maadhimisho haya kwa kutembelea shule moja, ili
kuhamasisha na kuongeza ari ya utendajikazi kwa walimu na wanafunzi wajisomee
kwa bidi.” Alisema Afisa Elimu Taaluma Bw. Rujuba.
Katika
risala yake ameihamasisha Jamii, kuwekeza katika Elimu kama hatua muhimu ya
kuzalisha nguvu kazi yenye ujuzi wa kulisaidia taifa lao, na kuongeza kwamba
uhamasishaji huo, umepelekea ofisi yake kuongeza idadi ya Wanafunzi 84,125
waliosajiliwa.
Amefafanua
kwamba idara ya msingi imefanya vizuri kitaaluma, ambapo katika mitihani ya darasa
la VII kitaifa kwa miaka mitatu tangu mwaka 2015 hadi 2017, imekuwa ya kwanza
kimkoa na imefanikiwa kuvuka lengo.
Maadhimisho
ya siku ya kilele cha wiki ya Elimu wilayani Ngara yameabatana na kuwatunuku vyeti walimu
wakuu, ambao shule zao zimefanya vizuri kitaaluma, ambapo shule tano za
sekondari na tano za msingi wametunukiwa vyeti hivyo.
Idara ya
Elimu Msingi katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara inazo shule 121, shule 115
ni za serikali, ambapo shule 06 ni za watu binafsi, na kwamba idara yake ina
walimu 1,373; walimu wa kiume ni 867 na wa kike 506.
|
No comments:
Post a Comment