
Mkutano wa Hadhara ukiendelea Kata ya Buhororo wilayani Ngara mkoani Kagera.Na Shaaban Ndyamukama-Radio Kwizera Ngara.
Jumla ya
Shilingi 70,000 zilizotolewa na Mpango wa kusaidia kaya maskini katika kijiji
cha buhororo wilaya ya Ngara mkoani Kagera, zinashikiliwa na uongozi wa kijiji
hicho kwa ajili ya kuwajengea nyumba walengwa wa fedha hizo baada ya kuonekana
kaya husika zinajihusisha na ulevi na
kuendekeza umaskini wao.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Buhororo Bw Staford Simon amesema hayo hii May 31,2018 wakati
wa mkutano wa hadhara ulioitishwa kwa ajili ya Diwani wa Kata ya Kibimba John
Shimimana kusikiliza kero za wananchi na kueleza mikakati ya kuwaletea
maendeleo.
Bw Simon amesema katika kijiji hicho kaya
tisa zinazonufaika na TASAF zimeonekana kutokuwa na matumizi bora ya fedha hizo
hivyo uongozi wa kijiji umeamua kupokea fedha zao na kuwanunulia vifaa vya
ujenzi wa makazi yao ambayo ni hayako katika ubora.

Awali mmoja
wa wakazi wa kijiji hicho Evelina
Prosper aliutaka uongozi wa kijiji kuwapatia elimu wanufaika wa tasaf
kuanzisha miradi ya kiuchumi kuepuka kuendelea kuitwa watu maskini.
Pia Mwenyekiti
huyo amemuomba Diwani kufuatilia serikalini kupata vibao ya usalama barabarani kuwekwa
katika kijiji hicho kutokana na kukithiri matukio ya ajali ambapo juzi
mwanafunzi wa pili amefariki shule ya msingi buhororo kwa kugongwa na gari.

Diwani wa Kata ya Kibimba.
Hata hivyo Diwani
wa Kata ya Kibimba John Shimimana amewataka wakazi wa kijiji katani humo kufanya kazi
badala ya wizi na ulevi kujiongezea umaskini.
Amesema kila
mmoja afanye kazi halali ambapo amekemea tabia ya kutorosha wanafunzi kwenda
kufanya kazi za ndani wilayani kahama ambapo wanafunzi wa buhororo shule ya
msingi na sekondari ya Kibimba waetoroshwa na baadhi kurudi baada ya kufanyiwa
vitendo vya ukatili huko kahama.
Aidha
amesema wananchi wajitahidi kuchangia ujenzi wa zahanati ya kijiji na
halmashauri ya wilaya iko katika mpango wa kusambaza maji mpaka kitongoji cha
Mubabwile mpakani na kijiji cha Kanazi.
Diwani wa
kata ya Kibimba yuko katika ziara ya kutembelea vijiji kusikiliza maoni na kero za wananchi lakini
kuwapatia utekelezaji wa mipango ya halmashauri ya wilaya hiyo.

Afisa Ugani wa Kata ya Kibimba.
Kwa upande
wake Afisa Ugani wa Kata ya Kibimba Juster
Julius amewataka wakulima wa kahawa kusubiria msimu wa mauzo ya zao hilo
katika vyama vya ushirika badala ya kuuzwa kwa walanguzi kuepuka faini au
kifungo.
Amesema
atakaye kamatwa akiuza kahawa kimagendo faini yake Shilingi milioni 8 au kifungo cha
miaka sita gerezani na watakaokaidi kutokomeza ugonjwa wa mnyauko watafikishwa
kwenye vyombo vya sheria.






No comments:
Post a Comment