|
Mkuu wa Mkoa
wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M.
Kijuu (Aliyesimama) Akitoa Maagizo ya Kuwasimamisha Kazi Watumishi Wawili Wilayani Karagwe.
Uamuazi wa
kuwasimamisha kazi watumishi wawili Afisa TEHAMA Bw. Beatus Nyarugenda na Mhasibu wa Mapato Bw. Innocent Kakulima ulitolewa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu katika kikao cha Kamati ya Fedha
cha Halmashauri hiyo ambapo alitoa maagizo kama ifutavyo;
MOJA, Uchunguzi wa kina ufanyike kwa kila
Maafisa walioomba na kuidhinisha marekebisho au miamala ya mapato ya ndani
katika mfumo bila kuwa na kibali cha Afisa Masuuli na kiasi cha fedha
kinachohusika katika eneo hilo ni Shilingi 427,027,430.49/=
PILI, Watumishi waliokusanya mapato na
hawajapeleka benki fedha walizokusanya jumla ya Shilingi 127,094,900/= hadi
tarehe 14 Aprili, 2018 waziwasilishe katika akaunti ya mapato ya Halmashauri
ndani ya siku 7, na vielelezo vihakikiwe na Katibu Tawala wa Wilaya ya Karagwe
na watakaoshindwa kutekeleza agizo hilo sheria ichukue mkondo wake.
TATU, Afisa TEHAMA Bw.Beatus Nyarugenda
tume ilimbaini kuwa hakuwa makini kwa kukiuka usalama wa mtandao kwa kutoa haki
kwa Afisa mmoja kukamilisha muamala mzima wa kufuta ama kubadili tarakimu za
fedha katika mtandao. Mkuu wa Mkoa aliagiza utaratibu huo uachwe mara moja na
Mkuu wa TEHAMA wa Mkoa kuhakikisha usalama wa mfumo unawekwa vizuri mara moja.
|
|
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi
na Usalama ya Wilaya ya Karagwe Wamkimsikiliza Mkuu wa Mkoa kwa Makini.
Baada ya
maagizo hayo Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu
alimwagiza Kamanda wa TAKUKURU Mkoa kupokea taarifa hiyo kwa ajili ya kuifanyia
uchunguzi ambao utatoa majibu sahihi ya kushuka kwa mapato ya Halmashauri ya
Wilaya ya Karagwe.
Aidha,
wakati uchunguzi unafanyika Mkuu wa Mkoa Mhe. Kijuu aliagiza Afisa TEHAMA Bw. Beatus Nyarugenda na aliyekuwa
Mhasibu wa Mapato Bw. Innocent Kakulima
wasimame kazi kupisha uchunguzi huo.
Pia aliagiza
kuwa wakati uchunguzi unaendelea watuhumiwa wengine watakaobainika kuwa
wanaweza kuingilia uchunguzi wawapo maeneo yao ya kazi ajulishwe haraka ili nao
wahusishwe kupisha uchunguzi.
Mkuu wa Mkoa
Mhe. Kijuu alihitimisha kwa kurudia
kumuagiza Kamanda wa TAKUKURU Mkoa kufanya Uchunguzi na kuukamilisha haraka pia
na kuzitahadharisha Halmashauri nyingine za Wilaya za Mkoa wa Kagera hususani Wakurugenzi Watendaji na Watumishi
wengine kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa bila kujihusisha na
vitendo vya kuyahujumu mapoto hasa mapato ya ndani ya Serikali.
|





No comments:
Post a Comment