Jamaal Tamimu awataka Vijana mkoani Kigoma kutumia Fursa zilizopo Kujikwamua Kiuchumi. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Monday, May 21, 2018

Jamaal Tamimu awataka Vijana mkoani Kigoma kutumia Fursa zilizopo Kujikwamua Kiuchumi.

Vijana 138 kutoka Shule za Msingi na Sekondari za wilaya saba za  mkoa Kigoma wapo kwenye Mafunzo ya Uskauti lengo likiwa ni kuimarisha ukakamavu wa miili yao na kupata umahili wa kiakili wakati wakiwa  kambini katika wilayani Kibondo mkoani Kigoma.

Picha/Habari Na-Shaaban Ndyamukama.
Vijana  katika Halmashauri za wilaya mkoani Kigoma wameshauriwa kutumia fursa za mkoa huo kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa wakitumia ardhi na rasilimali nyingine zinazopatikana mkoani humo.

Mlezi wa Vijjana wa wilaya ya Kibondo Jamaal Tamimu ambaye aliwahi kugombea Ubunge wa Jimbo la Kibondo kupitia Chama cha Mapinduzi  (CCM) alisema May 20, 2018 kwamba vijana hao wanahitaji kujituma katika kujikwamua kiuchumi pamoja na kujihadhari na vitendo vya uhalifu.

Alisema hayo wakati akihutubia   vijana 138 wa shule za msingi na sekondari kutoka wilaya saba za  mkoa Kigoma walipo kwenye mafunzo ya uskauti kuimarisha ukakamavu wa mwili na kupata umahili kiakili wakiwa  kambi katika wilayni Kibondo mkoani humo.

Alisema Serikali imeweka mkakati wa kuwanusuru Vijana hata wasio na ajira kuwahamasisha kujiunga kwenye vikundi kuanzisha miradi ya ki uchumi wakitumia vipaji vyao   badala ya kujiunga na  kushiriki vitendo vya  uhalifu na utumiaji wa madawa ya kulevya kasha kuvunja sheria wakiishia mikononi mwa vyombo vya dola.
Bw.Jamaal Tamimu.

“Taifa lolote linategemea vijana katika uzalishaji mali na kukuza uchumi hivyo tumieni fursa zinazopatikana katika mazingira yanayowazunguka  mkitumia fani zenye taaluma kufanya kazi kasha kujikwamua kiuchumi kuacha maisha tegemezi”Alisema Taminu

Pia alitumia fursa hiyo kuwapatia Shilingi 500,000 kuweza kuongezea mtaji katika miradi waliyoanzisha huku akisisitiza vijana kuheshimu na kutii mamaka zilizoundwa kisheria kudumisha amani na utulivu nchini.
Awali mmoja wa wananchama  wa maskauti wilaya ya Kibondo Anjelina Ernest alisema chama  cha Skauti wilayani Kibondo  chenye vikundi 106 katika shule za msingi na sekondari mkoani Kigoma wanachana na viongozi wao wanakabiliwa na changamoto ya  kukosa usafiri kuhudhuria vikao na mafunzo kujiongezea ujuzi na fani mbalimbali.

 Alisema chama hicho kimeanzisha mradi nyuki  kwa kumiliki mizinga 60 na kwamba mwezi  Julai vijana 40 wa  skauti mkoani Kigoma watahitaji kusafiri hadi nchini Rwanda kwa ajili ya kushiriki tamasha la Afrika mashariki kuonesha  kazi wanazozifanya.
Mratibu wa Makambi ya Skauti Mkoani KigomaThobias Huseni   alisema vijana wa skauti ni askari wa akiba ambao huchukua mafunzo ya chipukizi na hutumika katika shughuli mbalimbali za kijamii na kitaifa.

Alisema pia skauti wanafundishwa uzalendo, utii wa sheria, maadili ya kijamii lakini pia kuekekezwa kufanya kazi kulingana na nguvu zenye kurandana na umri wao ili kuwajengea tabia ya kujitegemea  kuanzia umri wa miaka 15 na kuendelea.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad