Yanga SC wafuzu Makundi Michuano ya CAF. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, April 19, 2018

Yanga SC wafuzu Makundi Michuano ya CAF.

April 19, 2018 Jumatano, Yanga SC imefanikiwa kukata tiketi ya kuingia hatua ya Makundi ya michuano ya CAF kwa kuitoa Waloitta Dicha ya Ethiopia katika hatua ya mtoano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

Yanga SC wakicheza ugenini Awassa Ethiopia katika mchezo wa marudiano wamepoteza kwa kufungwa bao 1-0 lililofungwa na Esheti Mena dakika ya 2 ila wanafanikiwa kufuzu kwa ushindi wa jumla ya mabao 2-1  baada ya mchezo wa kwanza nyumbani Tanzania ,Yanga SC walipata ushindi wa magoli 2-0 uwanja wa Taifa.
Baada ya matokeo hayo Yanga SC wanafuzu hatua ya Makundi ya michuano ya CAF kwa mara ya kwanza baada ya miaka miwili, mara ya mwisho Yanga SC kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo ilikuwa 2016, ambapo walipangwa na MO Bejaia ya Algeria, TP Mazembe ya Congo DRC na Medeama ya Ghana.

Yanga SC wamerudia rekodi yao ya mwaka 2016 ya kuingia hatua ya makundi ya michuano hiyo na waliingia hatua ya Makundi mwaka huo kwa kuitoa Sagrada Esperanca ya Angola kwa ushindi wa jumla ya magoli 2-1 licha ya mchezo wa marudiano kufungwa goli 1-0.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad