Taswira Picha zinaonesha hali ya baadhi ya maeneo Jijini DSM baada ya Mvua. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Tuesday, April 17, 2018

  Taswira Picha zinaonesha hali ya baadhi ya maeneo Jijini DSM baada ya Mvua.

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha jijini Dar es Salaam kuanzia mwishoni mwa wiki iliyopita zimesababisha mafuriko katika maeneo mbalimbali ya jiji huku watu kadhaa wakiripotiwa kufariki dunia kutokana na mvua hizo.

Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi, Lazaro Mambosasa amesema amepokea taarifa ya watu 9 kufariki dunia kutokana na mvua hizo huku wengine wakijeruhiwa.

Kamanda Mambosasa amesema vifo hivyo vimetokana na kuangukiwa na ukuta na wengine kusombwa na maji kutokana na mvua zilizonyesha kwa siku tatu mfululizo.


Aidha, mamia ya wakazi wa jiji hilo wameripotiwa kupoteza makazi yao kutokana na maafa hayo huku wengine wakipoteza mali zao.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amefika katika eneo la Jangwani April 16, 2018  na kushuhudia hali halisi, na kisha kutoa agizo kwa wakuu wa shule kuwa wanafunzi wapumzike nyumbani kwa siku mbili, mpaka hali itakapokuwa nzuri.

Makonda amewaomba wakazi waishio maeneo hayo kuchukua tahadhari na kuondoka maeneo hayo kwa kipindi hiki cha mvua ili kuepusha madhara makubwa zaidi kuwatokea.

BOFYA HAPAKUSOMA ZAIDI.







No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad