Taswira Picha Abiria walivyonusurika Kifo baada ya Basi la KIMOTCO Kupinduka ndani ya Mto. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Friday, March 16, 2018

Taswira Picha Abiria walivyonusurika Kifo baada ya Basi la KIMOTCO Kupinduka ndani ya Mto.

Basi la Kampuni ya KIMOTCO (pichani) lililokuwa likitoka Musoma,kwenda Arusha kupitia Mugumu,limepinduka katika mto unaodaiwa kuwa na viboko ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mhifadhi Mkuu wa hifadhi hiyo William Mwakilema amethibitisha kupata taarifa ya tukio hilo leo Machi 16,2018 na kusema kuwa katika ajali hiyo hakuna majeruhi wala vifo,na kuwa abiria wote walitoka ndani ya basi hilo na kukaa juu ya basi kusubiri msaada wa kuokolewa.

Jitihada za kuwaokoa mmoja mmoja zilifanyika.

Baada ya basi hilo kusombwa na maji abiria wote walitokea juu ya madilisha ya basi na kukaa juu yake,kwani halikuzama lote,jitihada za kuwaokoa zinaendelea  mpaka sasa,ambapo zaidi ya abiria wanne  wametolewa.

TAARIFA ZAIDI TUNASUBIRI KUTOKA MAMLAKA HUSIKA 
 Baadhi ya Abiria wakiwa juu ya basi hilo mara baada kupinduka,wakiokolewa mmoja mmoja na Lori kama ionekanavyo.
 

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad