
![]() |
Akitoa
Mahubiri katika ibada hiyo ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa
Katoliki mjini Rulenge, Askofu
wa Jimbo la Rulenge-Ngara Muhashamu Severine Niwemgizi amesema Jimbo hilo
limepata pigo la kuondokewa na Mosinyori Mutabazi kwani jimbo lilikuwa
likimtegemea kama mtafsiri wa biblia
Askofu
Niwemugizi amesema Mosinyori Emmanuel Mutabazi katika kipindi chote cha miaka
48 ya utume wake amekuwa akifanya kazi kwa bidii huku akiwaheshimu wakubwa na
wadogo.
|
![]() |
Hawa Masista ni Ndugu wa Marehemu Mosinyori Emmanuel Mutabazi waliposhiriki kuweka shada la maua wakati wa mazishi yake yaliyofanyika Juzi March 27,2018 katika makabuli ya Mapadre mjini Rulenge wilayani Ngara mkoani Kagera. |


![]() |
Kwa upande
wao waumini waliojitokeza kuuga mwili wa Mosinyori Mutabazi wamesema
wamempoteza mtu muhimu sana katika kanisa kutokana na wataendelea kumuenzi na
kumuombea kwa yote mema ambayo aliyafanya kwa maendeleo ya kiroho.
Mosinyori Emmanuel Mtabazi alikuwa mtaalam wa kutafsiri
biblia takatifu na Paroko msaidizi wa Parokia ya Chato mkoani Geita ambaye
alifariki alfajiri ya Marchi 25,2018.
|

No comments:
Post a Comment