Baada ya
Rayvanny na Dogo Janja katika Music Facts leo tungependa kukufahamisha machache
kuhusu Aslay.
Kupitia
Music Facts ya Bongo5 tunakusongezea mambo 8 ya kawaida kabisa kuhusu Aslay
ambayo ni kawaida kabisa na pengine si rahisi kuyabaini.
1.
Tangu
Aslay kuondoka Yamoto Band amemshirikisha msanii mmoja tu katika nyimbo zake,
naye ni Khadija Kopa katika wimbo uitwao Usitie Doa.
2.
Wimbo
mrefu zaidi wa Aslay ni Likizo, wimbo huu una dakika 4:29, pia wimbo mfupi
zaidi ni Baby ambao una dakika 3:09.
3.
Kwa
kipindi cha takribani miezi 11 iliyopita (Apr 10, 2017-Feb 22, 2018) Aslay
ametoa nyimbo zipatazo 15, sawa na wastani wa wimbo mmoja kila mwezi.
4.
Nandy
ameimba maneno mengi zaidi ya Aslay katika wimbo Subalkher, Nandy ameimba
maneno yapatayo 110 wakati Aslay ameimba maneno 108, ikiwa ni tofauti ya maneno
mawili.
5.
Twitter
ndio mtandao ambao Aslay ana followers wachache zaidi ukifuatia na facebook,
katika twitter ana followers 2K na Facebook 49K, Instagram ndio anaongoza kwa
kuwa followers Milioni 1.6.
6.
Wimbo
wa kwanza wa kundi la Yamoto Band ulijulikana kwa jina la Yamoto, verse ya
kwanza aliimba Aslay ila katika wimbo wa mwisho wa kundi hilo ‘Su’, verse ya
kwanza aliimba Beka Flavour na Aslay alikuwa wa msanii wa tatu kuimba kutoka
Yamoto Band baada ya Ruby ambaye walimshirikisha.
7.
Licha
ya kutoa ngoma mbili pamoja ‘Subalkher na Mahabuba’, Aslay hajawahi kumshiriki
Nandy katika wimbo wake wowote wala Nandy hajawahi kufanya hivyo,
kilichofanyika wameshirikiana tu.
8.
Wimbo
wa Aslay unaongozwa kwa kutazamwa zaidi katika mtandao wa YouTube ni Natamba.
Wimbo huu ulitoka October 4, 2017 na hadi sasa una views 5.5 YouTube.
(Bongo5)
|
No comments:
Post a Comment