Katika Hatua
nyingine Waziri Mwigulu alimwagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro
kutumia vyombo vyake vyote vya uchunguzi kuhakikisha anachunguza mauaji ya
wananchi katika maeneo mbalimbali nchini (Akitolea mfano wa Kijana aliyeuawa
Kinondoni wa chama cha CHADEMA) na baada ya uchunguzi Jeshi hilo litoe taarifa
kwa wananchi ili kujua chanzo cha mauaji hayo.
|
Kwaniaba ya
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Hamelore M. Manyanga ambaye ni Kamishna wa Huduma
za Sheria katika uzinduzi huo alitoa rai kwa wananchi kutoa taarifa sahihi
wakati zoezi la utambuzi na usajili wa Vitambulisho vya Taifa likiendelea. Pia
aliwaasa watendaji kuhakikisha wanajiepusha na vitendo vya rushwa katika zoezi
hilo vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuli kwa atakayebainika.
Aidha, Bw.
Alphonce Malibicha Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Vitambulisho vya Taifa
kwaniaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NIDA alisema kuwa wananchi wanaotakiwa
kusajiliwa ni umri kuanzia miaka 18 na kuendelea na raia wa Tanzania . Pia
alisema kuwa uandikishaji unaendelea katika Mikoa 19 sasa Tanzania Bara na
Kagera sasa imeongezeka baada ya kufanyika uzinduzi rasmi.
Bw.
Malibicha alizitaja faida za Vitambulisho vya Taifa kuwa ni pamoja na huduma
mbalimbali za kijamii, Vitambulisho vya Taifa vitatumika katika kusajili
Makampuni ambapo mmiliki taarifa zake lazima zionekane kwenye kitambulisho,
Vitatumika wakati wa kupata Hati ya kusafiria, Vitatumika katika mifuko ya
Hifadhi za jamii katika kutoa huduma za mafao kwa wananchama wake pia na
kubaini Wahamiaji Haramu.
|
Naye Mkuu wa
Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum M. Kijuu katika uzinduzi huo alitoa
maagizo kwa Watendaji wa ngazi zote kuhakikisha wanashiriki kikamilifu
kufanikisha zoezi la uandikishaji kwa kusimamia zoezi zima hasa Kamati za
Ulinzi na Usalama za Wilaya chini ya Wenyeviti wake Wakuu wa Wilaya.
Aidha, Mkuu
wa Mkoa Kijuu alitoa wito kwa watendaji kutojihusisha na vitendo vya rushwa
katika zoezi hilo kwani wakibainika hatua kali zitachukuliwa mara moja. Pia
aliwaasa wananchi kuhakikisha wahudhuria kujiandikisha kwa muda watakaopewa na
wasisubiri muda wa mwisho na kusababisha msongamano.
Mwisho Mh.
Kijuu aliwaomba viongozi wa dini kuwahamasisha waamini wao kujiandikisha kila
mmoja. Pia alisistiza kuwa zoezi la uandikishaji lisichukuliwe kidini wala
kisiasa kwa kuwapotosha wananchi na mwisho wake baadhi yao wakabaki bila
kujisajili na kupata Vitambulisho vya Taifa.
|
No comments:
Post a Comment