Naibu Waziri
wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Mhandisi Atashasta Nditiye akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nsele
kilichopo kata ya Kilondo wilayani Ludewa mkoani Njombe katika ziara yake ya
kukagua huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa
Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani
Njombe hadi Itungi wilayani Kyela mkoani Mbeya.
AIDHA Serikali ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetenga shilingi milioni 358 kwa ajili ya
kulipa fidia nyumba na ardhi za wananchi waishio mwambao wa Ziwa Nyasa kwa
ajili ya kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari za Ziwa hilo.
Katik ziara
hiyo, Meneja wa Mamlaka ya Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Msese
amesema kuwa Mamlaka ya Bandari Tanzania imetenga fedha hizo kwa ajili ya
kulipa fidia wananchi wa maeneo ya mwambao wa Ziwa Nyasa waliojitolea maeneo
yao ili kupisha upanuzi na ujenzi wa bandari zilizopo ndani ya Ziwa Nyasa
kuanzia bandari ya Lipingu iliyopo Wilaya ya Ludewa mkoa wa Njombe hadi bandari
ya Matema iiyopo wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.
Naye Mkuu wa
Wilaya wa Ludewa Bwana Andrea Tsere amemueleza Mhandisi Nditiye kuwa tayari
wamekamilisha kazi ya kuhakiki malipo ya fidia za wananchi waliotoa ardhi zao
eneo la Manda na Lupingu.
“Wanachi wa eneo la Manda watalipwa shilingi milioni
192 ambapo wametoa eneo la ukubwa wa hekari 24 na wa Lupingu wametoa eneo
ukubwa wa hekari 10.6 na watafidiwa shilingi milioni 166, amesema Tsere”.
Ujenzi wa
bandari hizo na utoaji wa huduma ya usafirishaji wa abiria na mizigo ni
ukamilishaji wa ahadi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli kwa wananchi waishio kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa ambao
wanategema Ziwa hio kwa kiasi kikubwa kwa shughuli za kiuchumi, biashara na
kijamii ambazo zitachangia ukuaji wa uchumi wa wananchi hao na taifa kwa
ujumla.
|
Meneja wa
Bandari za Ziwa Nyasa Bwana Ajuaye Heri Sese (wa pili kushoto) akifafanua jambo
kwa Naibu Waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Mhe. Mhandisi Atashasta Nditiye (wa pili kulia) wakati wa ziara
yake kuanzia kata ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi
wiliyani Kyela mkoani Mbeya. Wa kwanza kulia ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa Mhe.
Deo Ngalawa na wa kwanza kushoto ni Katibu wa Mhe. Nditiye Mhandisi Hamza
Faiswary.
|
Naibu Waziri
wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Mhandisi Atashasta Nditiye (aliyeketi) akisimikwa kuwa Chifu wa kitongoji cha
Ihiiga kilichopo kwenye kijiji cha Nkwimbili, kata ya Lupingu, Wilaya ya Ludewa
iliyopo mkoani Njombe ikiwa ishara ya pongezi kwa kiongozi wa kitaifa kufika
hapo tangu mwaka 1979 katika ziara yake ya kukagua huduma za mawasiliano na
maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa aliyoifanya kuanzia kata
ya Manda iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wiliyani Kyela
mkoani Mbeya. Wa kwanza kushoto ni mzee Thadei Otmari Ngalawa na aliyevaa
miwani ni Diwani wa Kata ya Lupingu Mhe. Skanda Mwinuka.
|
Mwenyekiti
wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ludewa Mzee Kolimba akimshukuru Naibu Waziri
wa Uchukuzi na Mawasiliano wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe.
Mhandisi Atashasta Nditiye (hayupo pichani) wakati wa ziara yake ya kukagua
huduma za mawasiliano na maeneo ya kujenga bandari kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa
aliyoifanya kuanzia kata ya Manda wilaya ya Ludewa mkoani Njombe hadi Itungi wilayani
Kyela mkoani Mbeya.
|
No comments:
Post a Comment