![]() |
Mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza akisoma
hotuba kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe katika
sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani zilizofanyika Mjini Dodoma.
Aidha
alipongeza kauli mbiu ya mwaka huu Redio na Michezo na kutoa rai kwa waandishi
wote wa habari kudumisha mila na desturi za Kitanzania na kuongea Kiswahili
fasaha bila kuchanganya na lugha zingine kama Kiingereza maarufu kama
Kiswanglish.
Aidha Waziri
Mwakyembe alishukuru Shirika la UNESCO na Mtandao wa Redio Jamii Tanzania
(TADIO) kwa kuwezesha siku ya redio na kusema atatafakari hoja zote
zilizowasilsihwa kwake.
Naye Katibu
wa Mtadao wa Radio Jamii (TADIO), Marco Mipawa akisoma hotuba kwa Niaba ya
Mwenyekiti wa Mtandao huo, Prosper Kwigize alitaka Serikali kuhakikisha kwamba
urasimu unaondolewa kwenye utoaji wa taarifa kwa umma ili kuwezesha kufanyika
kwa vipindi mbalimbali vya habari.
|
![]() |
Katibu wa
Mtandao wa Radio za Jamii nchini (TADIO), Marco Mipawa akisoma hotuba kwa niaba
ya Mwenyekiti wa Mtandao huo, Prosper Kwigize wakati maadhimisho ya Siku ya
Redio Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma kwa ufadhili wa UNESCO.
Alitaka
Tamisemi kuweka utaratibu wa utoaji habari katika mfumo rahisi ili wananchi
wafahamu kinachotekelezwa na serikali yao.
Aidha maafisa habari walioajiriwa
wapewe mamlaka na wawezeshwe kufahamu kinachofanywa na serikali na wawe na
ruhusa ya kutoa taarifa kwa vyombo vya habari katika maeneo yao.
Aidha
alisema kutokana kutokuwa na vyanzo vya mapato ya uhakika serikali ingeangalia
suala la kodi na ushuru mbalimbali ili kusaidia Redio za Jamii kutolipia huduma
za Radio.
Pia amesema
sheria zilizopo ukilinganisha na mazingira halisi ya kazi ya mwanahabari, mfano
sheria ya Takwimu, sheria ya huduma za habari, sheria ya makosa ya mtandao
kumeshabibisha tasnia ya habari na utangazaji kuwa katika mashaka zaidi kuliko
kipindi kilichopita.
Pia ameitaka
Serikali kutoa Ruzuku ya elimu au mafunzo ya kitaaluma kwa wanahabari ili
kuwawezesha kukidhi vigezo vya kisheria ifikapo 2021
|
![]() |
Kaimu Mkuu
wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo
(wa pili kushoto).
Kaimu Mkuu
wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo
amewataka waandishi na watangazaji kutumia redio kwa manufaa ya taifa kuleta
mshikamano na pia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo.
Aidha
alikumbusha historia ya redio na kazi iliyofanya duniani na kusema kwamba
umuhimu wa radio upo wazi na kutaka wahusika kuzitumia kwa manufaa ya umma
unaowazunguka.
Naye Mkuu wa
Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche
akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Dk
Moshi Kimizi, alitaka serikali na vyombo vya habari kushirikiana katika
kuhimiza michezo kwa kuwa ndicho kinachowaleta wananchi pamoja.
Alisema
anadhani redio na serikali vitaona njia bora ya kutangaza michezo kwa manufaa
ya taifa.
Awali
akimkaribisha Mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari Mh. Shonza, Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Dk. Binilith Mahenge amesema Unesco inafanya kazi nzuri sana kwa
kuwekeza kwenye vyombo vya Habari na kuvitaka vyombo hivyo kuitangaza Dodoma na
fursa zake kwa sababu ndio makao makuu ya nchi.
Aidha
aliitaka Redio kutangaza fursa zote ambazo zipo Dodoma ili wafanyakazi na
wafanyabiashara wanaohamia Dodoma kujua wanapata wapi mahitaji yao yakiwemo
Makazi, Maji, Chakula, Elimu na kadhalika.
Alitaka
vyombo hivyo kuvutia wawekezaji ili mji huo uwe kweli katika karne ya 21 na
makao makuu ya nchi.
|
![]() |
Mkuu wa
Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina Musaroche
akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Kaimu Katibu Mtendaji wa tume hiyo Dk.
Moshi Kimizi (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
yaliyofanyika Mjini Dodoma.
|
![]() |
Mkuu wa Mkoa
wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge akizungumza machache kabla ya
kumkaribisha mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo,
Mh. Juliana Shonza wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
yaliyofanyika mjini Dodoma.
Wa pili kulia ni Mgeni rasmi Naibu Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza, Kaimu Mkuu wa Ofisi za
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo (wa pili
kushoto) pamoja na Mkuu wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco
(NATCOM), Christina Musaroche (wa kwanza kushoto).
|
![]() |
Mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza
akiwasili katika hoteli ya Nashera mjini Dodoma kushiriki sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge (kulia) pamoja na Katibu wa Mtandao wa
Radio za Jamii nchini (TADIO), Marco Mipawa (kushoto).
|
![]() |
Kutoka kulia
ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge, Mgeni rasmi Naibu
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza, Kaimu Mkuu
wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Faith Shayo pamoja na Mkuu
wa Mawasiliano na Habari wa Tume ya Taifa ya Unesco (NATCOM), Christina
Musaroche wakiwa meza kuu wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio
Duniani mjini Dodoma.
|
![]() |
Mratibu wa
Mtandao wa Vyombo vya Habari na Jinsia Kusini mwa Afrika (GEMSAT) , Gladness
Munuo akitoa mada kuhusu usawa wa jinsia katika kuripoti michezo, changamoto na
taratibu zake wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
yaliyofanyika mjini Dodoma.
|
![]() |
Katibu wa
Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Neville Meena akisisitiza umuhimu wa maudhui
katika vipindi vya redio ambapo aliwaasa kutangaza masuala yanayowahusu
wanajamii katika maeneo yanayohusika badala ya kuwalisha wasikilizaji taarifa
ambazo ziko nje na mipaka wanayoishi.
|
![]() |
Mtaalamu wa
Vyombo vya Habari na Mawasiliano, Mariagoreth Charles akiwasilisha kanuni za
uandishi wa habari za mtandaoni na mitandao ya kijamii kwa waandishi wa habari
wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau
wengine wa habari nchini walioshiriki kwenye maadhimisho ya Siku ya Redio
Duniani yaliyofanyika mjini Dodoma.
|
![]() |
Mtangazaji
Mkongwe wa Habari za Michezo nchini, Abdallah Majura amesema pamoja na kwamba
waandishi wanatangaza vipindi vya michezo lakini maudhui hayakidhi na kuvutia
vile inavyostahili akitoa mfano hai wakati akichangia kwa nini waandishi wengi
hawaandiki habari za michezo. Majura amesema yeye mwenyewe amewahi kupata tuzo
mbili kwa ajili ya vipindi vya michezo.
|
![]() |
Pichani juu
na chini ni sehemu ya waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka
Tanzania Bara na Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini
waliohudhuria sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani yaliyofanyika
mjini Dodoma.
|










![]() |
Mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza (wa
tatu kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Dkt. Binilith Mahenge
(kushoto) pamoja na Kaimu Mkuu wa Ofisi za Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni
(UNESCO) nchini, Faith Shayo (wa tano kulia) wakicheza wimbo maalum wa
ngoma za asili wa Kikundi cha Kaza Roho cha mjini Dodoma ulioongozwa na Msanii
Mwinamila wakati wa sherehe za maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani
yaliyofanyika mjini Dodoma.
|
![]() |
Mgeni rasmi
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Juliana Shonza na meza kuu wakiwa katika picha ya pamoja na
waandishi wa habari wa vyombo vya habari vya jamii kutoka Tanzania Bara na
Visiwani pamoja na wadau wengine wa habari nchini wakati wa sherehe za
maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani February 13,2018 yaliyofanyika mjini Dodoma.
|
No comments:
Post a Comment