Jacob Zuma, ajiuzulu nafasi yake ya Urais wa Africa Kusini. - Mwana Wa Makonda

Muhtasari

X-BET


Post Top Ad

Thursday, February 15, 2018

Jacob Zuma, ajiuzulu nafasi yake ya Urais wa Africa Kusini.

Chama tawala nchini Africa Kusini cha ANC, kimepokea tangazo la kujiuzulu kwa Bw.Jacob Zuma katika nafasi yake ya Urais.

Akitangaza uamuzi huo,Bw. Zuma amesema asingependa damu imwagike na chama(ANC) kimeguke kwa sababu yake.

Afisa mmoja mwandamizi wa chama hicho amesema hatua hiyo italeta utulivu wakati nchi inakabiliwa na changamoto mbalimbali, Ameongeza kusema kuwa ANC haisherehekei hatua hiyo, kutokana na kwamba Zuma amekitumikia chama hicho kwa miaka 60.

Awali kupitia televisheni Bw. Zuma alisema hakubaliani na mahitaji ya uongozi wa ANC kwamba anapaswa kujiuzulu, lakini amejiuzulu ili kuepusha ghasia ambazo zingechafua jina lake.

Makamu wa Rais wa Africa Kusini Cyril Ramaphosa atapigiwa kura na wabunge kama mkuu wa nchi na baadaye kula kiapo ndani ya siku chache zijazo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad