Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara Yanga ya Dar es Salaam Wakiwa
ugenini katika uwanja wa Azam Complex, Mbande Chamazi kucheza mechi yake
ya 15 Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya wenyeji wao Azam FC.- imeibana
Azam FC na kuichapa kwa mabao 2-1 ushindi ambao umeipa Yanga pointi tatu na
kuifanya ifikishe pointi 28 na kubaki nafasi tatu ikiwa ni tofauti ya pointi
mbili na Azam ambayo ina pointi 30 katika nafasi ya pili huku ikiwa nyuma ya
Simba SC kwa Pointi nne.
Ushundi wa
Yanga SC umekuja wakati timu hiyo ikikabiliwa na idadi kubwa ya wachezaji wenye
majeraha (Yohana Mkomola, Pato Ngonyani, Thabani Kamusoko, Amis Tambwe, Donald
Ngoma, Abdallah Shaibu ‘Ninja’ na Pius Buswita ambaye alikuwa anatumikia kadi
tatu za njano).
Mechi
nyingine za Ligi Kuu leo January 27, 2018, Mwadui FC imelazimishwa sare ya 2-2
na Njombe Mji FC Uwanja wa Mwadui Complex, Shinyanga, Mbeya City imelazimishwa
sarte ya 0-0 na Mtibwa Sugar Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya na Kagera Sugar
imetoka 0-0 na Lipuli FC Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.
|
No comments:
Post a Comment